News
Loading...
Image Map HII NI 24 RADIO SIKILIZA NA UTUTUMIE SMS KWENDA 0684 666320 KUHUSU UNAVYOTUSIKIA

Thursday 27 July 2017

ACHEZEA KIPIGO CHA MBWA MWIZI KUTOKA KWA BELLA BAADA YA KUELEZA UKWELI KWAMBA ALIFANYA SHOW KAIMBIA VITI TUPU CONGO!!


Mwimbaji wa kujitegemea wa miondoko ya rumba Jimmy Manzaka amedai kuangushiwa kipigo na wafuasi wa Christian Bella kwa kile anachoamini kuwa ni wivu kutokana na ujio wake wa nyimbo mbili kali. Manzaka raia wa Congo ambaye amekuwa akifanya shughuli za muziki huko Dubai, yupo Tanzania kwa miezi kadhaa akipika albam yake ya rumba ambapo tayari ameachia nyimbo mbili “Shilawadu” na “Coco Channel”. Mwimbaji huyo mwenye undugu na Nyoshi el Saadat anadai kipigo hicho kilitokea takriban siku kumi zilizopita Sinza jijini Dar es Salaam nyumbani kwa Christian Bella. Manzaka anadai alikwenda kumtembelea Nyoshi ambaye anaishi jirani na Christian Bella ambaye amedai pia kuwa wanafahamiana vizuri. Jimmy Manzaka anasema baadae alikaa kwenye pub moja ya jirani akipata kinywaji na rafiki zake na ndipo alipomuona Bella akirejea nyumbani kwake hivyo akaamua kwenda kumsalimia kwa kuwa ni rafiki yake. “Bella alikuwa anarejea safari kutoka nje ya Dar, nikaenda kumsalimia, tukaongea vizuri kisha nikarejea pub kuendelea kunywa na rafiki zangu, lakini muda mfupi baadae akaja mtu na kuniambia kuwa Bella ananiita nyumbani kwake,” anaeleza Jimmy Manzaka katika mazungumzo yake na Saluti5. “Baada ya kufika nyumbani kwake Bella akaanza kunishutumu kuwa mimi namsema vibaya kwa watu, namtangazia kuwa alikosa watu kwenye show zake za Bukavu, Congo. “Nikajaribu kujitetea lakini haikusaidia, watu wake wakanikaba na kuanza kunipiga huku Bella akisema yeye ndiyo mwenye Dar es Salaam, yeye ndiyo rais na anaweza kunifanya lolote kwa kuwa mimi ni mshamba na siwezi kushinda na yeye,” alifunguka Jimmy Manzaka ambaye pia alionyesha picha zake zenye makovu sehemu za shingoni kuthibitisha kile alichofanyiwa nyumbani kwa Bella. Hata hivyo Bella alipoulizwa na Saluti5 juu ya tuhuma hizo, alisema hizo ni kiki za kijinga. Bella anasema hajawahi kumwalika nyumbani kwake Jimmy Manzaka kwa kuwa hawana ukaribu huo na wala sio rafiki yake. “Kama anasema alipigwa nyumbani kwangu basi aeleze vizuri alikwenda kufanya nini. Sijawahi kumwalika kwangu, kama alijipeleka mwenyewe na kukutana na wasaidizi wangu wasiomfahamu, hiyo mimi sina namna ya kumsaidia,”anaeleza Bella. “Wasaidizi wangu waliniambia kuna mtu mlevi aliingia ndani kwa nguvu na kulazimisha kuonana na mimi, wakambwambia Bella hayupo lakini bado akawa mbishi kutoka, wakamtoa nje kwa nguvu, sijapewa taarifa kuwa mtu huyo alipigwa,” anafafanua Bella na kuhoji ni vipi mtu aingie kwa nguvu nyumbani kwa mtu kama njia za kutafuta kiki. “Kama kweli alipigwa basi aseme amechukua hatua gani, alikwenda kuripoti kituo kipi cha polisi, alitibiwa hospitali gani. Kwangu mimi hizo naziona ni kiki za kizamani sana, atafute njia nyingine ya kutokea,” anaeleza Christian Bella kupitia maongezi ya simu
Share on Google Plus

About

0 comments :

Post a Comment