HAJI MANARA RASMI AELEZEA HABARI ILIYOZAGAA MTANDAONI YA SIMBA KUFUNGWA 7-0
Baada ya Taarifa Kuzagaa kwenye Mitandao kuwa Simba Ilicheza Mchezo wa Kirafiki na Kufungwa bao 7 Kwa 0 wametoa Taarifa Kwa Vyombo vya Habari.
Juhudi zangu za kumtafuta Haji Manara zilizaa matunda na kuniambia hata yeye aliziona pia kupitia mtandao na kuamua kulitolea ufafanuzi rasmi kama Club Taarifa yenyewe ni kama ifuatavyo
Klabu ya Simba kwa masikitiko makubwa inakanusha taarifa potofu zinazosambaa mitandaoni na kwenye baadhi ya vyombo vya habari,kuwa imecheza mechi ya kirafiki nchini Afrika kusini,na kupoteza mchezo huo.
Uzushi huo unasema Simba imefungwa mchezo huo kwa jumla ya goli 7-0, na timu ya daraja la kwanza ya nchini humo, Royal Eagles.
Kiukweli Simba haina rekodi za hovyo kama hizo kokote inapocheza duniani,na haijawahi kufungwa na klabu yoyote idadi ya magoli kama hayo,kama zilivyo klabu nyingine nchini,hususan klabu ambayo mashabiki wake ndio wanaozusha upuuzi huo.
Dunia ya leo ni ya Teknolojia, na ingekuwa ni kweli,hakuna mtanzania ambae asingeiona hii taarifa kutoka kwenye mitandao au vyombo vya habari vya Afrika kusini.
Tunapenda Umma wa watanzania utambue kwa siku zote tulizokuwa huko,program ya benchi la ufundi, ilijikita ktk kuitengeneza miili ya wachezaji kistamina.
Wiki ijayo Timu yetu inatarajiwa kucheza mechi mbili na klabu za Orlando Pirates na Bidverst za nchini humo, kabla ya kurejea tarehe tano mwezi ujao teyari kwa mchezo wetu wa SIMBA DAY utakaopigwa tarehe nane mwezi ujao.
Mwisho
Tunawaomba wanachama na mashabiki wetu puuzeni uzushi wa mitandaoni, na taarifa rasmi zitatolewa kwa mujibu wa taratibu rasmi za klabu.
IMETOLEWA NA..
HAJI S MANARA
MKUU WA HABARI WA SIMBA SC
SIMBA NGUVU MOJA
0 comments :
Post a Comment