News
Loading...
Image Map HII NI 24 RADIO SIKILIZA NA UTUTUMIE SMS KWENDA 0684 666320 KUHUSU UNAVYOTUSIKIA

Friday 28 July 2017

TETESI ZA USAJILI KUTOKA VYANZO MBALIMBALI MCHANA HUU 28 JULY 2017


TETESI ZA USAJILI MANCHESTER UNITED 28 JULY 2017 (28.7.2017)
Jose Mourinho ameonyesha Utayari wa Kutaka Kumsaini Mchezaji Gareth Bale toka Real Madrid, mara baada ya Madrid Kuonekana nguvu kubwa Kuiweka kwa Kinda Kylian Mbappe toka Monaco, Kocha wa Real Madrid Zidane amesema Anataka kumbakiza Bale lakini atalazimika Kumuuza.(Mail Sports)

Mchezaji aliyekuwa akiwindwa na Manchester United na Chelsea Radja Nainggolan amemaliza Utata kwa Kuongeza Mkataba wa miaka minne kutumikia Romaya Italia. 

Mchezaji Ivan Perisic huenda akapewa Ofa mpya na Inter Milan, Mchazaji huyo ni mmoja kati ya wachezaji wanaomtoa Udenda Kocha wa Manchester United Jose Mourinho. (The sun)

Manchester United wako tayari Kuongeza Pesa itakayowatamanisha Chelsea kuwaachia Nemanja Matic, Hii inakuja siku kadhaa toka Chelsea watangaze kutowauzia United Mchezaji Huyo. (The Sun)

TETESI ZA USAJILI CHELSEA 28 JULY 2017 (28.7.2017)

Chelsea  wameingia katika mchakato wa Kumsaka Alex Oxlade Chamberlain na Mchezaji wa Everton Ross Barkley. (Hii ni Kulingana na Telegraph).

Kocha wa Chelea ameweka wazi kuwa Chelsea wameshindwa kumnasa Kyle Walker, Huku akisema Kama angeambiwa amchague Mshambuliaji Bora kwasasa Uingereza angemchagua Harry Kane.

LIVERPOOL KUHUSU NABY KEITA  NA TETESI 28.7.2017
Klabu ya Liverpool inajipanga Kufanya Jaribio la Mwisho kwa Naby Keita ambaye amekuwa akimtoa Udenda Kocha Jurgen Klopp. (Mirror)

Barcelona  Wanataka kumtumia Rakitic kama kishawishi cha Liverpool kuwaachia Mchezaji Phillipe Couinho, Yani Barca wanataka Wawape Liverpool mchezaji huyo na Kisha kuwaongezea pesa Kiasi hii ni Kulingana na Vyombo vya habari nchini Hispania 


USAJILI WA NEYMAR WA BARCELONA  KWENDA PSG 28.7.2017
PSG wamewaomba Barcelona kushusha Bei ya Kumuuza Neymar Jr. Dos Santos, Bei inayotajwa Kuuzwa Neymar ni pauni milioni 195. (The Sun). 
Share on Google Plus

About

0 comments :

Post a Comment