Kipa wa Azam FC, Aishi Manula. |
Inadaiwa kuwa Manula ameshamalizana na Simba kwa mkataba wa miaka miwili lakini hataweza kutangazwa rasmi kuwa mchezaji wa timu hiyo kwa kuwa bado mkataba wake na Azam FC haujamalizika.
Taarifa ambazo gazeti hili limezipata ni kuwa uongozi wa Simba umeiomba Azam FC kumruhusu Manula mapema ili akafanye mazoezi na kikosi hicho kilichopo Afrika Kusini ili kuepuka kesi kama ilivyokuwa kwa Hassan Kessy alivyokwenda Yanga.
Ulipotafutwa uongozi wa Azam FC kuzungumzia suala hilo ulisema kwa upande wao wanatambua kuwa Manula ni mchezaji wao hadi pale atakapomaliza mkataba na si vinginevyo.
“Manula bado ni mchezaji wetu hadi atakapomaliza mkataba wake, pia yeye mwenyewe ndiye anatakiwa aseme kama amemaliza mkataba ama la, lakini taarifa za Simba kufanya mazungumzo bado hazijanifikia,” alisema Mwenyekiti wa Azam FC, Idrisa Nassor.
Stori: Khadija Mngwai | Championi
0 comments :
Post a Comment