Klabu ya Yanga kupitia kwa Mwenyekiti wa kamati ya Usajili Hussein Nyika ameulizwa kama Yanga wameshamalizana na mchezaji " Fundi " kiungo wa Kati wa Mbeya City Raphael Alpha Daudi na Nyika amesita Kumtangaza Rasmi.
Nyika amesema Watu Wasubiri maana anapenda Kutangaza Vitu ambavyo vinakuwa vimekamilika, Kwasasa Nyika Yuko mjini Morogoro kwaajili ya Kufanya mazungumzo na Kocha George Lwandamina ili kuangalia Mapengo yaliyobaki waweze kumaliza Kazi.
Nyika amesema Yanga ikimtaka Mchezaji yeyote Yule wanauwezo wa kumpata na kwao hela siyo Tatizo kabisa.
![](https://is05.ezphotoshare.com/2017/07/17/snRRYI.jpg)
![](https://is02.ezphotoshare.com/2017/07/23/sAYGYx.jpg)
0 comments :
Post a Comment