HUKU hivi karibuni alishafanikiwa kupata watoto mapacha, Eva na Matthew na mwingine akiwa njiani, straika wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo, ametangaza kuwa angependa kuwa baba wa watoto saba.
Staa huyo wa Real Madrid aliyasema hayo juzi katika mahojiano na chombo cha habari nchini Ureno, Vidas akiwa nchini China ambapo pamoja na mambo mengine alielezea mipango hiyo ya kuongeza familia.
“Kuhusu watoto ninaowataka ni saba, ni namba ya miujiza na ninaikubali vizuri,” alisema Ronaldo
![](https://is05.ezphotoshare.com/2017/07/17/snRRYI.jpg)
![](https://is02.ezphotoshare.com/2017/07/23/sAYGYx.jpg)
0 comments :
Post a Comment