News
Loading...
Image Map HII NI 24 RADIO SIKILIZA NA UTUTUMIE SMS KWENDA 0684 666320 KUHUSU UNAVYOTUSIKIA

Wednesday 12 July 2017

MCGREGOR AMSHINDA MAYWEATHER MAPEMA KABLA YA PAMBANO

MAI2
Bondia Conor McGregor ameahidi kumshinda Mpinzani wake Floyd Mayweather ndani ya Raundi nne katika Pambano lao litakalofanyika Agosti 26 Mwaka huu Mjini Los Angels nchini Marekani.
MAI
Mayweather,4o pamoja na McGregor  wamekutana kwa mara ya Kwanza Mjini Los Angels katika Mkutano mbele ya Waandishi wa Habari na mamia ya watu huku wakijinadi na kutambia kabla ya Pambano lao la kihistoria la uzito wa Kati.
“Miguu yake midogo, akili yake ndogo na Kichwa chake kidogo. Ntampiga ndani ya Raundi ya nne, atapoteza fahamu mapema tu, Mwendo wake na anavyoonekana hataniweza kabisa”. Alisema Bondia McGregor mbele ya Mamia ya watu na waandishi wa Habari.
Kwa upande wake Bondia Floyd Mayweather ambaye ni Mshindi mara tano wa Ubingwa wa Dunia kwa Uzito wa Kati amesema Licha ya umri wake na kuonekana amechoka ameahidi kumshinda McGregor ambaye hajawai pigana Pambano la Kimataifa.
Floyd Mayweather na Conor McGregor wanakutana kwa mara ya kwanza Ulingoni katika Pambano lao litakalopigwa Agosti 26 mwaka huu 2017 Mjini Los Angels nchini Marekani. Mayweather atashuka kwenye Pambano hilo akiwa na Historia ya kutopoteza Mchezo wowote huku Conor McGregor akiwa amepoteza Michezo mitatu katika Michezo 26 aliyocheza.

Share on Google Plus

About

0 comments :

Post a Comment