Add caption |
Marekani. Kocha wa Tottenham amemjia juu mwamuzi baada ya timu yake kuzamishwa mabao 3-2 dhidi ya Roma kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa jana Jumanne kwenye Uwanja wa Red Bull Arena, Jersey nchini Marekani.
Pochettino alionekana akimlaumu mwamuzi kwa kile alichodai kuwa mechi hiyo ingeisha kwa sare ya mabao 2-2 lakini kitendo cha kufungwa bao la tatu kulisababisha kocha huyo kushindwa kujizuia na kuonyesha hasira zake kwa mwamuzi wa mchezo huo.
Maofisa usalama wa timu walisogea kumtuliza kocha Pochettino ambaye alikuwa na jazba baada ya timu yake kufungwa bao la tatu.
0 comments :
Post a Comment