Kwenye mtandao leo habari kubwa sana ni kwamba eti timu ya simba jana ilicheza mechi ya kujipima nguvu South Africa ambapo imeweka kambi yake na Habari hiyo inaenda mbali zaidi ikisema kwamba kwenye mtanange huo timu ya Simba imekula wiki au seven o'clock yani 7-0 japo mpaka sasa taarifa hizo hazijathibitishwa na Viongozi wa Timu ya simba wala ushahidi wa mechi hio, nilinyanyua simu yangu kumpigia msemaji wa timu ya Simba bwana Haji Manara lakini simu yake imeitaa muda mrefu bila kupokelewa kwa sasa najaribu kuwatafuta Watanzania waishio South Africa wanipe ukweli wa swala hilo ili kuwapasha ukweli wa hali ya mambo wapenzi wasomaji wa blog hii pendwa lakini mpaka sasa hili swala linaonekana kama ukweli wake ni mdogo kwa kua Dunia ya sasa ni Dunia ya utandawazi hakuna kinachoweza kujificha hasa kwa timu kubwa kama ya Simba icheze alafu watu wasijue kaeni mkao wa kula swala hili ntaliweka wazi muda mchache tu ntakapopata ukweli wa mambo
0 comments :
Post a Comment