KWA mwonekano Wallace Karia hana tofauti na raia wengi wa Somalia,
ninamaanisha Wasomali. Ninaamini wako viongozi wengi wa soka, serikalini
na sehemu mbalimbali wana mwonekano kama raia wengine wa Somalia na
suala la kwamba ni raia wa Tanzania, halina shaka hata kidogo.
Anayeweza kufanya kazi ya kukagua fulani ni raia au la, ni Idara ya
Uhamiaji na si vinginevyo. Kawaida watu wanaweza kuwa na asili tofauti
za nchi mbalimbali na wakawa Watanzania kama ilivyo kwa Karia ambaye ni
mmoja wa wagombea wa nafasi ya urais katika uchaguzi wa Shirikisho la
Soka Tanzania (TFF) utakaofanyika Agosti 12, mwaka huu.
Karia ni mtumishi wa serikali na aliwekewa pingamizi wakati wa usaili
wa uchaguzi huo, kwamba si raia. Mwisho aliyeweka pingamizi, alishindwa
kuthibitisha alichokipinga na Karia ambaye ni Makamu wa Rais wa TFF,
ambaye sasa anakaimu nafasi ya urais wa shirikisho hilo, akapitishwa.
Lakini kwa sasa inaonekana suala lake linataka kugeuka na kuwa
mjadala mkuu wa uchaguzi mkuu wa TFF badala ya sera na mambo sahihi
ambayo wapenda mpira au wataka maendeleo ya mpira wangependa kuyasikia.
Wanaogombea wakiwemo wanaochuana na Karia, wanaonekana kutaka
kuligeuza suala hilo ni silaha na mbaya zaidi hata wale ambao hawakuweka
pingamizi wanaling’ang’ania na kutaka liwe mjadala mkuu. Kama kweli
kuna mtu ana uhakika Karia si raia, ni vizuri akaliļ¬ kisha suala hilo
sehemu husika na baada ya hapo aliache walifanyie kazi kwa kuwa wao
ndiyo wanataalamu wa uhakika wa kujua fulani ni raia au la tena kwa
uhakika badala ya taarifa za mitaani. Karia alisisitiza ni raia wa
Tanzania ingawa alikubali ana asili ya Somalia.
Sasa kama kuna anayejua zaidi, vizuri akawasaidia Idara ya Uhamiaji
kama raia mwema ili wafanye kazi yao. Lakini suala la uchaguzi, vizuri
mkajikita na nini mtafanya na mtaleta maendeleo yapi katika mchezo wa
soka. Hakika kikubwa wadau tunaangalia nani ataleta maendeleo na hili
ndiyo jambo kubwa zaidi kuliko rangi, kabila au jambo fulani la mtu.
Suala la uadilifu linaweza kuwa muhimu pia kwa kuwa tumeona namna
viongozi wengi walio kwenye mpira ambavyo wamekuwa wakitafuna fedha za
mpira bila ya aibu hata kidogo na wengi wamekuwa wakiona kama ni haki
kufanya hivyo na wanapozuiwa au kukosolewa basi wanaona kama wanaonewa
au kudhalilishwa.
Tuwe na haya, tuone aibu kwa kuwa viongozi mliopita na wengi mpo
mnagombea TFF mmeuumiza sana mpira wetu mkiwa katika klabu au hata
shirikisho. Basi safari hii lazima mjue watu wanataka maendeleo,
wanataka mabadiliko na hivyo wekeni sera, semeni mtaleta nini kuliko
kung’ang’ania hoja ambazo hazihusu mpira na kuzigeuza hoja zinazotemewa
au zitakazoujenga mpira wa Tanzania ambao unahitaji msaada na watu
sahihi kuliko blabla.
0 comments :
Post a Comment