News
Loading...
Image Map HII NI 24 RADIO SIKILIZA NA UTUTUMIE SMS KWENDA 0684 666320 KUHUSU UNAVYOTUSIKIA

Monday 24 July 2017

HII NDIO TAARIFA RASMI KUTOKA TFF KUHUSU SAKATA LA SIMBA KUPOKONYWA NAFASI BAADA ZA ZANZIBAR KUPOKONYWA UANACHAMA CAF


Baada ya kuwepo Taarifa zilizozagaa kwenye Mitandao ya Kijamii Kuhusu Simba Kupokonywa Nafasi ya uwakilishi wa Kombe la Shirikikisho mara baada ya Zanzibar Kupokonywa Uanachama na CAF,

Kulingana na Taarifa hizo   zilieleza kuwa Bingwa wa Tanzania Bara atashiriki Klabu Bingwa Afrika na Bingwa wa Zanzibar atashiriki Kombe la Shirikisho Afrika nafasi ambayo Simba ndiyo nafasi Yake.

Lakini Leo Afisa Habari wa TFF Alfred Lucas Amesema " Kwanza Niseme Kitu Kimoja Taarifa hizo ni za Uongo, Kaimu rais na kaimu katibu Mkuu wa TFF hawajatoa Statement yeyote, na mimi sijatoa chochote kwahiyo kilichokuwa Kinazungumzwa ni Uongo na nawaomba wanafamilia wa Mpira wa Miguu waitupilie mbali Taarifa Hiyo " 

Alimaliza Kwa Kusema Hivyo Afisa Habari wa TFF Alfred Lucas ambaye amekanusha Vikali Taarifa Hizo
Share on Google Plus

About

0 comments :

Post a Comment