News
Loading...
Image Map HII NI 24 RADIO SIKILIZA NA UTUTUMIE SMS KWENDA 0684 666320 KUHUSU UNAVYOTUSIKIA

Sunday 30 July 2017

HABARI MBAYA!! CHAZ BABA APATA AJALI MBAYA YA GARI!!

Mwimbaji star wa dansi Chaz Baba, amenusurika kifo baada ya kupata ajali mbaya ya gari leo alfajiri. Chaz Baba amepata ajali hiyo kilomita chache kutoka Singida mjini akiwa njiani kuelekea Nzega ambapo gari lake aina ya Toyota Porte limeharibika vibaya. Mwimbaji huyo ameieleza Saluti5 kuwa hakujua nini kilichotokea kwasababu alikuwa amesinzia huku gari likiwa linaendeshwa na rafiki yake. “Nilishtuka baada ya gari kuacha njia na kwenda kuparamia mawe makubwa. Mwenzangu aliyekuwa akiendesha gari aliniambia kuwa alifanyiwa mchezo mchafu wa kupewa ‘bodi’ na gari kubwa na kupelekea kuingia maporini,” anaeleza Chaz Baba. Chaz anasema yuko salama ingawa ameumia maeneo kadhaa.



credit sallut5

Share on Google Plus

About

0 comments :

Post a Comment