News
Loading...
Image Map HII NI 24 RADIO SIKILIZA NA UTUTUMIE SMS KWENDA 0684 666320 KUHUSU UNAVYOTUSIKIA

Sunday 30 July 2017

KUTUPIA PICHA FB KWAMPONZA JOHN TERRY WAZEE WA KAZI WAMWINGILIA NA KUMSAFISHA!! PICHA ZA TUKIO ZIMA HAPA!! NA WEZI WENYEWE HAWA HAPA!!

wanaume wa kazi wakiwa wamebeba  mzigo tayari kwa kutoroka eneo la Tukio
NI jambo la kawaida wachezaji wanapokuwa mapumziko baada ya ligi mbalimbali kumalizika, kwenda kula bata katika maeneo ya kifahari na kisha kutupia picha kwenye mitandao ya kijamii wakionesha jinsi wanavyotanua wakiwana na familia zao.
Hata hivyo, licha ya kuwa kwao wanaona ni ujiko kuonesha jinsi wanavyokula na kuponda raha, lakini kwa upande mwingine huwa hawafahamu wanaziweka rehani mali zao walizoziacha nyuma.

wezi waliomuingiza mjini John Terry

Na hivi ndivyo ilivyomtokea nahodha wa zamani Chelsea, John Terry, baada ya kujikuta akikombwa vito vya thamani wakati akiwa kwenye mapumziko.
Tukio hilo lilitokea mapema mwaka huu baada ya kundi la majambazi kuvamia jumba lake la kifahari lenye thamani ya pauni milioni 5 ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 14.5 za Kitanzania na kisha wakaondoka na vito vya thamani ya pauni 400,000 ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 1.2 ikiwa ni baada ya staa huyo kutupia picha zake kwenye mtandao wake wa Instagram zikimwonesha akiwa mapumziko.
Wanaume wa kazi wakiingia ndani kwa Terry
Picha hizo katika mtandao huo wa Terry katika Instagram, ndizo zinazodaiwa kuwashawishi majambazi hao hadi wakaamua kuvunja nyumba hiyo iliyopo katika eneo la Georgia lililopo Oxshott, Surrey.
Inaelezwa kuwa hata hivyo ni kawaida ya Terry, 36 na mkewe Toni, kuonyesha picha za mjengo huo ambao ulikuwa unamilikiwa na nyota wa zamani wa gofu, Colin Montgomerie, kwenye mtandao huo wa kijamii tangu walipoanza kuumiliki na hivyo ndivyo ilivyotokea baada ya kutupia picha hizo na kuonwa na wafuasi wake wapatao milioni 3.4, kundi hilo likatinga likiwa na shoka na kubomoa mlango na kisha likaondoka na mzigo huo wa vito vya thamani.
wanaume wa kazi wakiwa wamebeba  mzigo tayari kwa kutoroka eneo la Tukio

Katika tukio hilo, majambazi hao waliondoka na mkufu wa dhahabu wenye thamani ya pauni 219,000, pete yenye thamani ya pauni 61,000, kitabu chenye thamani ya pauni 18,000 ambacho kilikuwa ni toleo la kwanza la mtunzi, Harry Potter, kilichokuwa chumbani kwa Terry.
Hata hivyo, inaelezwa kuwa kutokana na wingi wa vito vya thamani vilivyokuwamo ndani ya mjengo huo hawakuweza kuondoka navyo vyote na hadi sasa hakuna kilichopatikana.
Taarifa zinaeleza kuwa baada ya majambazi hao kuondoka na mzigo muda wa saa 9 alfajiri, kengele ya kuashiria hatari ilianza kulia ndipo wakakimbia na polisi walipofika eneo la tukio wakakuta hata zuria lake lenye thamani ya pauni milioni 19,000 na samani zake za ndani zikiwa zimeharibiwa.
 
Mbali na hilo, vile vile maofisa hao wa polisi walikuta zana nzito ambazo zinasadikika ndizo walizozitumia kuvunja na kuingia ndani ya chumba cha Terry ambako anahifadhi vito hivyo.
Taarifa hizo zinaeleza kuwa baada ya kufanya uchunguzi polisi waliweza kuwatambua wanaume watano kupitia kamera za CCTV zilizokuwa karibu na nyumba ya staa huyo pamoja na kituo cha mafuta kilichopo jirani.

Wanaume hao ambao leo watahukumiwa kwenye Mahakama ya Kingston kutokana na tukio hilo lililotokea Februari 25, mwaka huu ni Darren Eastaugh, 30, Joshua Sumer, 27, Roy Head, 28 na Oliver Hart, mwenye umri wa miaka 25 kwa kosa hilo la kuiba kwa kutumia nguvu.
Katika kesi hiyo, jambazi mwingine wa tano, Kye Hardy-King, 25 yeye anakabiliwa na kosa la kuhifadhi vifaa vya kufanyia uhalifu baada kukutwa nyumbani kwake.
Vifaa hivyo vinadaiwa kutumika kufanya uhalifu katika matukio saba yaliyotokea katika maeneo ya Surrey na Sussex mapema mwaka huu ambapo waathirika walipoteza mali zenye thamani ya pauni 600,000.

Mwathirika mwingine ambaye naye alivamiwa wiki chache baada ya Terry kuibiwa ni mfanyabiashara mashuhuri Alfie Best, ambaye ufahamika kwa jina maarufu kama ‘gypsy king’ aliyepoteza vito vya thamani ya pauni 150,000.
Share on Google Plus

About

0 comments :

Post a Comment