Wakati ukijiandaa kushuhudia uhondo wa Ligi Kuu England ukiendelea, hizi hapa rekodi ambazo pengine hujawahi kuzisikia.
5. Hat-trick mipira ya adhabu
‘Set pieces’ ndio jina linalotumika kwenye soka wakati mpira unapohusisha frii kiki au penalti kiki. Hivyo basi, straika Wayne Rooney mwaka 2011 na gwiji wa Southampton, Matt Le Tissier mwaka 1995 walifunga hat-trick zao kwa mipira ya aina hiyo, ambapo wakali hao kwenye mechi zao walizocheza.
Siku ambayo walifunga mara tatu, walifanya hivyo kwa mipira ya set pieces.
4. Mechi isiyokuwa na kona
Anza kushangaa matokeo ya mechi hii. Wigan ikiwa nyumbani ilikubali kipigo cha mabao 6-0 kutoka kwa Chelsea mwaka 2010: Mechi hiyo imeingia kwenye kitabu cha historia ya Ligi Kuu England kwa jambo moja tu, hakuna mpira wowote wa kona uliopigwa katika mchezo huo licha ya mtu kupigwa nyingi. Hakuna mechi nyingine kwenye Ligi Kuu England ambayo ilichezwa kwa dakika zote 90 isitokee kona hata moja.
3. Kipa mshambuliaji
Unamkumbuka Paul Robinson? Huyu alikuwa kipa, ambaye alijipatia umaarufu mkubwa kwenye Ligi Kuu England wakati alipocheza kwenye vikosi vya Leeds United, Tottenham na Blackburn Rovers.
Lakini, kipa huyo ameweka rekodi ya kuwa mshambuliaji hatari zaidi. Robinson si alikuwa akifunga mabao tu kwenye Ligi Kuu England, bali ametoa asisti tano pia huku akiwahi kupata penalti kwa kuchezewa rafu ndani ya boksi la timu pinzani. Pamoja na kutokuwa mwenye namba ya kudumu ndani, lakini alikuwa akisumbua akicheza nafasi hiyo.
2. Wachezaji wagoma kutoka
Katika msimu wa 2002/03, Manchester United iliyokuwa ikifukuzia ubingwa iliikaribisha Fulham kwenye Uwanja wa Old Trafford. Katika mechi hiyo, Man United ilishinda bila presha 3-0, siku ambayo straika wake Ruud Van Nistelrooy alipiga hat-trick. Wakati mechi ikiendelea makocha wote walitaka kufanya mabadiliko kutoa wachezaji, matokeo yake hakuna mchezaji aliyetaka kutoka, mechi hiyo haikuwa na sub yeyote.
Hii ndiyo mechi pekee ambayo hakuna timu iliyofanya sub.
1. Kadi nyekundu bila kugusa mpira
Kama ulikuwa hujui, kwenye historia ya Ligi Kuu England kuna wachezaji watatu walionyeshwa kadi nyekundu ikiwa hata hawajagusa mpira.






0 comments :
Post a Comment