News
Loading...
Image Map HII NI 24 RADIO SIKILIZA NA UTUTUMIE SMS KWENDA 0684 666320 KUHUSU UNAVYOTUSIKIA

Saturday, 30 December 2017

KINACHOKWAMISHA ASANTE KWASI KUCHEZA SIMBA NI HIKI HAPA…



Kuchelewa kupata leseni za kuwaruhusu kucheza kwenye timu zao mpya walizojiunga nazo kwenye dirisha dogo la usajili, kunaweza kumfanya beki mpya wa Simba, Asante Kwasi kulazimika kusubiri michuano ya Kombe la Mapinduzi ambayo imeshaanza visiwani Zanzibar.
Taarifa kutoka Simba zinaeleza kuwa wameshindwa kwenda na Kwasi Mtwara kwenye mechi ya Ligi ya Vodacom kwa sababu Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), halijatoa leseni ya kumruhusu kuichezea timu hiyo.
"Tumekamilisha kila kitu lakini bado leseni ambayo siyo tatizo letu ni la TFF, wenyewe kwahiyo kwa kuhofia kupokwa pointi kama tutamtumia nivyema tukamweka pembeni na kuanza kumtumia rasmi kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi, " alisema Kapinga.
Hiyo inamaana kuwa Kwasi atajiunga na kikosi cha Simba, mara baada ya timu kurejea Dar es Salaam kikitokea Mtwara na atakuwa miongoni mwa kikosi cha wachezaji wa timu hiyo kitakachokwenda Zanzibar kushiriki michuano ya Mapinduzi Simba wakiwa makamu bingwa baada ya kumaliza nafasi ya pili mapema mwaka huu.
Katika michuano hiyo ya Mapinduzi, Simba imepangwa Kundi A ikiwa pamoja na Azam FC, URA ya Uganda, Jamhuri na Mwenge wakati Kundi B lina timu za Singida United, Yanga SC, Zimamoto, Mlandege, JKU na Taifa ya Jan’gombe.
USISAHAU KULIKE PAGE YETU HAPA
Share on Google Plus

About

0 comments :

Post a Comment