News
Loading...
Image Map HII NI 24 RADIO SIKILIZA NA UTUTUMIE SMS KWENDA 0684 666320 KUHUSU UNAVYOTUSIKIA

Saturday, 23 December 2017

ILE ISHU YA TSHISHIMBI KUMTWANGA MCHEZAJ MWENZAKE WA YANGA ILIKUA HIVI!!


YANGA ama kweli hawataki utani kwa jinsi wachezaji wanavyopambana katika mazoezi kuwania namba katika kikosi cha kwanza, kiasi cha kusababisha wachezaji kushikana mashati pale mmoja wapo anapodhani kufanyiwa ndivyo sivyo.
Ni kutokana na hali hiyo, kiungo wa timu hiyo, Papy Kabamba Tshishimbi, alijikuta akimpiga ngumi Seleman Yusuph baada ya kinda huyo kuonekana kumchezea ndivyo sivyo mwenzake huyo kwenye mazoezi yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam jana.
Yusuph alijikuta akirushiwa konde hilo kiaina na Tshishimbi akidaiwa ‘kumwingia mzima mzima’ mchezaji mwenzake huyo kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) aliyeonekana kuhofia kuumizwa tena mguu wake, hivyo kufanya hivyo kama njia ya kujihami.
Katika tukio hilo, Tshishimbi alikuwa na mpira, wakati akitafuta mtu wa kumpasia, ndipo akatokea Yusuph akamwingia mguuni kwa nguvu na kumlazimu nyota huyo kuhamaki na kumpiga kinda huyo ngumi ya kimtindo ambayo hata hivyo, wasimamizi wa mazoezi hayo, kocha msaidizi Shadrack Nsajigwa alimaliza tukio hilo kiaina na mazoezi kuendelea kama kawaida
USISAHAU KULIKE PAGE YETU HAPA
Share on Google Plus

About

0 comments :

Post a Comment