Mshambuliaji raia wa Ufaransa Lacazette anaekipiga na Arsenal ataikosa mechi muhimu dhidi ya Manchester United baada ya kuumia nyonga katika mchezo wa jana jumatano dhidi ya Huddersfield.
Arsenal katika mchezo huo wakicheza soka safi waliweza kuibuka na ushidi wa goli 5-0 ikiwa ni onyo kwa mashetani hao wa Old Traford watakaokutana nao jumamosi hii. Alexndre Lacazette dakika tu ya tatu ya mchezo akipokea pasi nzuri ya Ramsey aliweza kufunga goli zuri na kuwatanguliza mbele Arsenal likiwa goli lake la saba katika ligi .
Lacazette alitolewa kipindi cha mapumziko baada ya kuumia na nafasi yake kuchukuliwa na Olvier Giroud aliyeweza kuwapa Arsenal magoli mawili akiwa katika kiwango bora zaidi.
Magoli mengine ya Arsenal yalifungwa na Mesut Ozil na Alex Sanchez


0 comments :
Post a Comment