News
Loading...
Image Map HII NI 24 RADIO SIKILIZA NA UTUTUMIE SMS KWENDA 0684 666320 KUHUSU UNAVYOTUSIKIA

Thursday, 30 November 2017

MASHABIKI YANGA HAWATAKI MCHEZO : WAAMUA KUISAIDIA TIMU KUMTIBU KAMUSOKO



Baada ya kusota nje kwa muda mrefu mashabiki wa klabu ya Yanga wamejitolea kumtibu kiungo mshambuliaji Thabani Kamusoko ili kuipigania timu yao.
Kundi la mashabiki wa Yanga, wamejitolea kuisaidia timu yao kwa kumtibu kiungo wa Zimbabwe Thabani Scara Kamusoko, ambaye yupo nje kwa muda mrefu akisumbuliwa na tatizo ya goti.
Taarifa kutoka kwa mmoja wa madaktari ambao wanamapenzi makubwa na klabu hiyo, amesema wamejipanga kuhakikisha wanamaliza tatizo la Kamusoko ili aweze kurudi uwanjani kwa ajili ya kuitumikia timu yao pindi ligi itakapoendelea baada ya michuano ya Chalenji kukamilika.
"Nikweli kama watu wenye mapenzi mema na Yanga, tumeona nivyema tukaisaidia klabu yetu baadhi ya majukumu, likiwemo hili la kumtibia Kamusoko, aweze kupona tatizo lake ambalo limemuweka nje kwa muda mrefu," imesema taarifa hiyo.
Daktari huyo amesema zoezi hilo wanatarajia kulikamilisha kipindi hiki ambacho ligi ipo kwenye mapumziko mafupi na tunataka itakapoendelea aweze kurudi uwanjani na kuisaidia timu kuweza kutimiza malengo ambayo wameyapanga msimu huu.
Kamusoko ameichezea Yanga, mechi mbili tangu kuanza kwa msimu huu na  kupatwa na tatizo hilo, ambalo limemfanya kukosa mechi saba za ligi ya Bara, inayoendelea na klabu imekuwa ikimfanyia matibabu lakini hali yake inaonekana bado haijatengemaa ipasavyo.

USISAHAU KULIKE PAGE YETU HAPA
Share on Google Plus

About

0 comments :

Post a Comment