News
Loading...
Image Map HII NI 24 RADIO SIKILIZA NA UTUTUMIE SMS KWENDA 0684 666320 KUHUSU UNAVYOTUSIKIA

Wednesday, 25 October 2017

KIPIGO CHA 3-0 CHA ABAJALO CHAMPOTEZEA MAISHA KOCHA: ALIANZA KULIA KISHA AKADONDOKA NA KUPOTEZA MAISHA


Rashid Mahadhi amefariki dunia ikiwa ni muda mfupi baada ya timu yake ya Abajalo kupoteza mechi dhidi ya Changanyikeni. Mechi hiyo ilichezwa kwenye Uwanja wa Tandika jijini Dar es Salaam na Abajalo kutoka Sinza maarufu kama Mnyama ikapoteza kwa mabao 3-0. Baada ya kipigo hicho, Mahadhi aliangua kilio hali akisema wachezaji hawakuonyesha juhudi na wakati mwingine alionekana kutofurahishwa na maamuzi. Baadhi ya watu wa Ajabalo walilazimika kumtoa eneo hilo la uwanja na kumuingiza vyumbani huku akiendelea kulia. Lakini baadaye ilielezwa, hali yake ilizidi kuwa mbaya baada ya presha kupanda, akaanguka. Juhudi zilifanyika kumkimbiza hospitali, lakini baadaye alifariki dunia. Mahadhi alikuwa akimsaidia Kocha Abdallah Kibadeni ambaye kila alipopata nafasi alikwenda kutoa ujuzi wake kwa timu hiyo ya mtaani kwao. Abajalo ni timu ya mtaani kwa Kibadeni na Mahadhi ambao wanaishi nyumbani jirani Sinza kabla ya kuhama. Mahadhi ambaye ni mtoto wa nyota wa zamani wa soka, pia ni kaka wa kiungo wa zamani wa Yanga, Waziri Mahadhi 'Mendieta'. MWENYEZI MUNGU AMREHEMU.

USISAHAU KULIKE PAGE YETU HAPA
Share on Google Plus

About

0 comments :

Post a Comment