Msemaji wa klabu ya Simba, Haji Manara ameendelea kumuandama nyota mpya wa klabu ya Yanga raia wa Congo, Papy Kabamba Tshishimbi.
Papy Tshishimbi amejiunga na Wana jangwani akitokea klabu ya Mbabane Swallows inayoshiriki Ligi Kuu ya nchini Swaziland.
Kupitia akaunti yake ya instagram, Haji Manara ameposti picha ya Tshishimbi na ya mwanamuziki wa Tanzania, Shilole, na kuambatanisha maneneo ya utani kwa nyota huyo wa Yanga kuwa iweje Mwanaume na Mwanamke wakafanana majina.
"Daah huyu Shilole vp?huyo ni mwanamme ww demu,vp mtumie jina moja?au ndo vile tena!!" ameandika hivyo msemaji huyo , Haji Manara
Baada ya post hio ya Manara watu wengi walitoa maoni yao wakisema Haji Manara anamkosea heshima Mchezaji huo kwa kua kama utani umepita kiwango na anapaswa ajielewe kwamba kwa kua yeye ni msemaji wa Club basi ajue neno lake ni sauti ya Club hivyo wamemtaka aachane na mambo ya ajabu mtandaoni kwa kua itakuja kumletea matatizo
kumjadili chizi aliye timuliwa cuf alafu akahamia ccm na kutapeli kiasi cha pesa ni ujinga mawazo yake ndipo yalipo komea hapo kulingana na hali yake
ReplyDelete