News
Loading...
Image Map HII NI 24 RADIO SIKILIZA NA UTUTUMIE SMS KWENDA 0684 666320 KUHUSU UNAVYOTUSIKIA

Monday, 4 September 2017

HABARI MPYA ZA SASA HIVI KUTOKA YANGA NIMEKUWEKEA HAPA ZOTE "2" ZISOME HAPA!!

   Tokeo la picha la yanga sports club


NJOMBE MJI YAMFANYIA MAZOEZI RASMI TSHISHIMBI

Njombe Mji inayonolewa na Kocha Hassan Banyai itakuwa mwenyeji wa Yanga katika mchezo wa ligi kuu utakaopigwa wikiendi hii kwenye Uwanja wa Sabasaba, Njombe. 

Katika mchezo wa kwanza uwanjani hapo Njombe walifungwa mabao 2-1 na Prisons ya Mbeya.

 Mmoja wa viongozi wa Njombe Mji ameliambia Championi Jumatatu kuwa, lengo la kujiandaa kuwazuia mastaa wa Yanga ni kuhakikisha wanaambulia hata pointi moja kwa mabingwa hao watetezi wa ligi kama walivyofanya majirani zao Lipuli FC ya Iringa. 

“Tunajua kuwa Yanga wana mastaa wanaofanya vizuri katika ligi akiwemo kiungo wao mpya, Papy Kabamba Tshishimbi lakini sisi nikwambie tu tunajiandaa vizuri kuhakikisha tunawazima hao na kutokuwa na madhara mbele yetu.

 “Tumepania tupate hata pointi moja kwenye mechi hiyo kama lengo letu la pointi tatu litafeli, tunataka kuona tunafanya vizuri katika mchezo huo,” alisema kiongozi huyo ambaye hakutaka jina lake litajwe.

WASHAMBULIAJI wa kutumainiwa wa Yanga, Obery Chirwa pamoja na Amissi Tambwe leo hii wataungana na kikosi hicho katika mazoezi ya kujiandaa na mechi yao ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Njombe Mji katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. 

Yanga na Njombe Mji zitapambana Jumamosi hii katika Uwanja wa Sabasaba mijini Njombe baada ya Shirikisho la Soka Tanzania kuifanyia mabadiliko ratiba ya ligi kuu ambapo awali ilikuwa zipambane Jumatano hii. Kitendo hicho cha nyota hao kujiunga na kikosi hicho kimepokelewa kwa mikono miwili na viongozi wa benchi la ufundi la timu hiyo baada ya kuwakosa kwa kipindi kirefu kutokana na kusumbuliwa na majeraha ya goti. 

Majeraha hayo yaliwafanya wawe nje ya uwanja kwa kipindi kirefu huku wakishindwa kuitumikia timu yao hiyo katika mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba lakini pia ule wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Lipuli FC. Mechi zote hizo Yanga haikufanya vizuri. Akizungumza na mwanasports leo Blog, Daktari wa Yanga, Edward Bavu, alisema kuwa wachezaji hao kwa pamoja leo hii wataanza mazoezi baada ya kupona majeraha yao. 

“Hakika tunamshukuru Mungu kwa hilo kwani wamerejea katika kipindi muafaka baada ya kupona majeraha yao ya goti. “Kwa hiyo, mpaka kufikia hapa kazi iliyobakia ni kwa makocha kuhakikisha wanawapatia mazoezi ya ufiti kabla ya kuanza kuwatumia katika mechi zijazo,” alisema Bavu na kuongeza: “Wachezaji ambao tutaendelea kuwakosa kikosini kwetu ni kipa Beno Kakolanya na Geofrey Mwashiuya ambao wote bado ni majeruhi na wanaendelea na matibabu.” 


* USISAHAU KULIKE PAGE YETU HAPA* Millionaire  Ads
Share on Google Plus

About

0 comments :

Post a Comment