News
Loading...
Image Map HII NI 24 RADIO SIKILIZA NA UTUTUMIE SMS KWENDA 0684 666320 KUHUSU UNAVYOTUSIKIA

Friday, 1 September 2017

SHANGAA HII!! MC CONOR PAMBANO 1TU NA KADUNDWA VIZURI LAKINI HELA ALIYOPATA AMEMFUNIKA RONALDO MAPATO YA MWAKA MZIMA


Tokeo la picha la mayweather vs mcgregor TKO
Baada ya kupigana pambano la kitajiri, bondia Conor McGregor ameingia kwenye orodha ya wanamichezo walioingiza mkwanja mwingi ndani ya mwaka huu akimzidi hata staa wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo.
Katika pambano lake dhidi ya Floyd Mayweather, wiki iliyopita, McGregor aliingiza pauni milioni 77 (Sh bilioni 171) ndani ya usiku mmoja. Ronaldo alikuwa akiongoza mastaa wa michezo walioingiza fedha nyingi kwa kuingia pauni milioni 71 (Sh bilioni 157) kwa mwaka.
Tokeo la picha la mayweather vs mcgregor TKO
Hivyo, kutokana na rekodi hiyo, ripoti ikitoka mwisho wa mwaka huu McGregor atakuwa juu ya Ronaldo. Upande wa Mayweather hakamatiki kwa kuwa hadi sasa atakuwa ameshaingiza pauni 233m (Sh bilioni 518), hivyo bila shaka atakuwa namba moja kwa mwaka 2017.
* USISAHAU KULIKE PAGE YETU HAPA*
Share on Google Plus

About

0 comments :

Post a Comment