Mara baada ya Manchester United kupangwa kundi moja na CSKA Moscow ya Urusi katika Ligi ya Mabingwa Ulaya imeelezwa kuwa United itawalipia mashabiki wake gharama za visa kuingia kwenye nchi hiyo.
United itasafiri Septemba 27 kwenda Urusi kucheza dhidi ya wapinzani wao na hivyo shabiki yeyote ambaye atahitaji kusafiri kutoka England kwenda kushuhudia mchezo huo atalipiwa Visa ambayo gharama yake ni pauni 118.20 (Sh 262,000).
Hatua hiyo imefikiwa baada ya maombi kutoka kwa Chama cha Mashabiki wa Manchester United (M.U.S.T) kutokana na utaratibu wa malipo kuwa makubwa kuingia Urusi. Msimu uliopita United ilifanya hivyo kwa mashabiki wake 238 wakati wa mchezo dhidi ya Rostov.
* USISAHAU KULIKE PAGE YETU HAPA*

0 comments :
Post a Comment