Florida, Marekani. Mcheza tenisi Serena Williams amejifungua salama mtoto wa kike leo.
Serena (35), alisema alipelekwa katiak hospitali West Palm Beach, Florida jana kabla ya kuingizwa katika chumba cha kujifungulia usiku wa kuamkia leo.
Amepata mtoto wa kike leo, kwa mujibu wa taarifa ya America's WPBF-25, produzya wake Chris Shepherd alitweeted habari njema.
Katika mtandao wake wa kijamii aliandika: "nyota wa tenisi Serena Williams amejifungua mtoto wa kike akiwa na uzito wa 6 pounds 13 ounces.
"Mama na mtoto wote wanaendelea vizuri."
Aliongeza kuwa: "Taarifa ya kujifungua kwa Serena Williams ameipata kutoka vyanzo ndani ya hospitali hiyo."
Huyo ni mtoto wa kwanza kwa Serena akiwa na mchumba wake Alexis Ohanian mwenye miaka 33 na mmoja wawaanzishi wa Reddit .

0 comments :
Post a Comment