News
Loading...
Image Map HII NI 24 RADIO SIKILIZA NA UTUTUMIE SMS KWENDA 0684 666320 KUHUSU UNAVYOTUSIKIA

Saturday, 2 September 2017

HII NDIO HABARI RASMI KUTOKA TFF JUU YA ZULLU NA YANGA: NANI KAKENUA NA YUPI KANUNA? SOMA HAPA!!

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limefanikiwa kumaliza mgogoro wa kimasilahi kati ya wakala wa aliyekuwa kiungo wa Yanga, Mzambia, Justin Zullu ‘Mkata Umeme’, Muisrael, Karin Nir na uongozi wa Yanga, kufuatia kukatisha mkataba wa kiungo huyo.
TFF imemaliza suala hilo baada ya wakala wa kiungo  huyo Jumatatu ya wiki hii kupeleka mkataba wa mteja wake katika shirikisho hilo lengo likiwa ni kuzuia Yanga kuendelea kumtumia kiungo mpya raia wa DR Congo, Papy Tshishimbi pamoja na kwenda Fifa kufungua kesi ya madai kutatishwa kiholela mkataba wa Mkata Umeme.
Baada ya kufika TFF, uamuzi ulifanyika wa kuita pande mbili za mchezaji huyo na Yanga ambapo kwa pamoja wamemalizana vizuri na kila mtu ameondoka akiwa ameridhika japokuwa hakuna taarifa zaidi kutoka ndani licha ya kuwa awali Zullu alipanga kuishitaki Yanga kwenye Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).
Ikumbukwe kuwa, Novemba, mwaka jana, Yanga iliingia mkataba wa mwaka mmoja na Zulu mbele ya wakala wake huyo raia wa Israel, lakini hivi karibuni ilitangaza kuachana na kiungo huyo kutokana na kiwango chake kutowaridhisha.
Ikumbukwe, Mkata Umeme alipanga kuishitaki Yanga katika Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) ili alipwe dola 100,000 (Sh milioni 221)  kwa kuwa Yanga walivunja mkataba wake kiholela
* USISAHAU KULIKE PAGE YETU HAPA* Millionaire  Ads
Share on Google Plus

About

0 comments :

Post a Comment