Mshambuliaji mpya wa Simba, Nicholaus Gyan ashametua kutua nchini leo hii tayari kwa kuungana na wenzake kisha
kujiandaa na mechi ya Ligi Kuu bara dhidi ya Azam FC.
Gyan ambaye mwanzoni mwa mwezi ulipotia alitua nchini kwa ajili ya kumalizana na Simba kisha kutambulishwa katika Tamasha la Simba Day alirudi kwao Ghana kumalizana na timu yake aliyokuwa akiitumikia.
Kocha wa Simba, Joseph Omog ameshusha pumzi baada ya kupewa taarifa za kurejea nchini kwa Gyan ambaye ataiongezea nguvu safu yake ya ushambuliaji ambayo hadi sasa ina mabao saba.
Akizungumza na mwanasports leo Jumamosi, Omog alisema: “ ni jambo zuri kwetu kwani ataiongezea nguvu safu yetu ya
ushambuliaji kwa ajili ya kukabiliana na Azam.
“Gyan yupo vizuri aliyonyesha uwezo mkubwa tulipocheza na Rayon Sports (ya Rwanda katika Simba Day) kwa hiyo ni matumaini yangu atatusaidia katika mechi hiyo na nyingine zinazokuja.”
* USISAHAU KULIKE PAGE YETU HAPA*

0 comments :
Post a Comment