London, England. Manchester City imekasirishwa na kitendo kilichofanywa na viongozi wa Arsenal kukwamisha uhamisho wa mshambuliaji Alexis Sanchez usiku wa kuamkia leo.
Gunners waliamua kubaki na Sanchez baada ya kushindwa kukamilisha uhamisho wa Thomas Lemar kutoka kwa Monaco.
Lemar aliwaonyesha mashabiki wa Arsenal kitu gani watakikosa kwa kufunga mabao mawili ya kwanza wakati Ufaransa ilikisambaratisha Uholanzi kwa mabao 4-0 katika mchezo wa kusaka kufuzu kwa Kombe la Dunia 2018.
Arsenal ilifanya jitihada kubwa kutaka kumsajili chipukizi huyo mwenye miaka 21, kwa uhamisho ambao ungevunja rekodi ya klabu hiyo wa pauni 92milioni, lakini uhamisho huo ulishindikana kufanyika katika dakika za mwisho.
Ilikuwa ikiaminika kuwa Lemar alitaka kwenda Liverpool ili apate nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa.
Kukwama kwa uhamisho wa Lemar ndicho kikwazo kwa mshambuliahi wa Chile, Sanchez kujiunga na City usiku huo.
City inasemekana ilikuwa tayari kutoa pauni 60milioni kwa Sanchez ambaye sasa amebaki Arsenal hadi mwisho wa msimu mkataba wake utakapokwisha.

0 comments :
Post a Comment