
WAKATI wa Ligi Kuu Tanzania Bara ikitarajiwa kuendelea tena leo Jumatano, Yanga imebainisha wazi kwamba haisumbuliwi na mahasimu wao Simba kuongoza msimamo huo, kwani wanawaona kama wametangulia na
baiskeli ya miti. Aidha Yanga wamesema pamoja na Simba kuwa kileleni wana uhakika mwisho wa Ligi hiyo wao ndio watakaoondoka na Kombe la Ligi Kuu kama ilivyo ada yao, kwani wanaanza taratibu. Kwa mujibu wa msemaji wa Yanga, Dismas Ten wao hawana chembe yoyote ya hofu, kwani kutokana na kikosi bora ambacho wanacho msimu huu, wana uhakika mkubwa wa kufanya vizuri. "Sisi kwetu ni jambo la kawaida mno kuona kwamba tumeanza Ligi vibaya, lakini nakuhakikishia kwamba, wenzetu wanatangulia na baiskeli ya miti sisi tunawakuta tu na tutawapita," alisema. Yanga ilianza msimu huu mpya wa Ligi Kuu kwa kulazishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Lipuli ya Iringa ambayo imepanda daraja msimu huu kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar-es salaam.
* USISAHAU KULIKE PAGE YETU HAPA*

0 comments :
Post a Comment