News
Loading...
Image Map HII NI 24 RADIO SIKILIZA NA UTUTUMIE SMS KWENDA 0684 666320 KUHUSU UNAVYOTUSIKIA

Monday, 4 September 2017

HABARI MUHIMU KWA WAPENZI NA WANACHAMA WA SIMBA KUTOKA KWA MSEMAJI MKUU WA SIMBA HAJI MANARA


Klabu ya Simba, leo Jumatatu imeitangaza Kamati Maalum itakayohusika na kumtafuta mzabuni ambaye atanunua hisa 50% za timu hiyo katika suala lake la uendeshaji mpya wa klabu hiyo.

Kamati hiyo itaundwa na wajumbe watano na itaongozwa na Mwenyekiti wake, Jaji Mstaafu, Thomas Mihayo sambamba na wajumbe wanne ambao ni Wakili Damas Ndumbaro, Mbunge wa Ilala, Azzan Zungu, Yussuf Majjid Nassor na Abdulrazak Badru ambaye ni Mkurugenzi wa Bodi ua Mikopo ya Elimu ya Juu Tanzania.

Kamati itakutana Alhamisi wiki hii kuanza kazi ya kuwajadili wanachama ambao watataka kuzinunua hisa hizo ambapo watafuata sheria za manunuzi ya umma ambapo watakaa kwa siku 45 kabla ya kumtangaza mzabuni wa timu hiyo.



* USISAHAU KULIKE PAGE YETU HAPA* Millionaire  Ads
Share on Google Plus

About

0 comments :

Post a Comment