mwamuzi anamliza mchezo, wachezaji wote wanapongezana.
Dakika ya 94: Mtibwa wanafanya mabadiliko, mchezaji anayetoka anatoka tararibu.
Dakika ya 93: Juma Makapu wa Yanga anapewa kadi ya njano kwa kucheza vibaya.
Dakika ya 93: Presha anaendelea kuwa kubwa kwa Mtibwa, Yanga wanapambana kutafuta bao.
Dakika ya 91: Wachezaji wengi wa Mtibwa wamereudi nyuma kuzuia.
Dakika ya 90: Mwamuzi wa akiba anaonyesha dakika 4 za nyongeza,.
Dakika ya 89: Bado mambo ni magumu kwa kila upande
Dakika ya 85: Mwashiuya anaumia, yupo chini anatibiwa.
Dakika ya 84: Yanga wanafanya shambulizi kali, inakuwa kona lakini inakuwa haina faida.
Dakika ya 83: Mechezo umekuwa na kasi kubwa kwa timu zote
Dakika ya 80, Mwashiuya anaingia vizuri, anaachia mkwaju mkali kabisa hapa, mpira unamzidi nguvu Tinnoco, unagonga mwamba na Baba Ubaya anaondoa hatari.
Dakika ya 79: Ngoma anatoka, nafasi yake inachukuliwa na Mahadhi.
Dakika ya 78: Ngoma yupo chini ameumia, anapatiwa matibabu.
Dakika ya 75: Yanga wanafanya shambulizi kali lakini Ngoma na Ajibu wanashindwa kumalizia kazi nzuri waliyoifanya.
Dakika ya 73 Kipa Tinnoco wanafanya kazi ya ziada kuokoa shuti la mwisho la Buswita baada ya shambulizi kali la Yanga katika kipindi cha pili
Dakika ya 71, Daud anakwenda nje kwa upande wa Yanga na nafasi yake inachukuliwa na Geofrey Mwashiuya
Dakika ya 69: Beki wa Yanga, Gadiel Michael anapewa kadi ya njano kwa kuunawa mpira akidhani umetoka.
Dakika ya 65: Presha imekuwa kubwa kwa Yanga, Mtibwa wanafika langoni mwa Yanga mara kadhaa.
Dakika ya 62: Mtibwa wanapata kona nyingine.
Dakika ya 59: Mtibwa wanapata kona lakini wanashindwa kuitumia vizuri.
Dakika ya 56: Yanga wanafanya mabadiliko, anatoka Obrey Chirwa ambaye mchezo wa leo umemshinda na nafasi yake inachukuliwa na Kamusoko ambaye anaingiza kuimarisha kiungo.
Dakika ya 55, Mtibwa wanagongeana vizuri na kufanya mashambulizi mawili makali likiwemo shuti la Mbonde ambalo Rostand analitema. Sasa Mbonde yuko chini anatibiwa.
Dakika ya 51: Pius Buswita anawatoka mabeki wa Mtibwa, anaachia mkwaju mkali hapa kipa anaokoa hapa
Dakika ya 51: Ibrahim Ajib anawachambua vizuri hapa mabeki wa Mtibwa, lakini pasi yake ya mwisho inakuwa mkaa
Dakika ya 49: Mtibwa Sugar wanamtoa Hassan Dilunga na kumuingiza Kelvin Sabato Kongwe ambaye ni mshambuliaji
Dakika ya 50: Kasi ya mchezo inaongezeka.
Dakika ya 46: Mchezo umeanza kwa timu zote kusomana.
Kipindi cha pili kimeanza.
Timu zinaingia kwa ajili ya kipindi cha pili.
MAPUMZIKO
Timu zote zinaelekea vyumbani kupumzika.
Dakika ya 47: Mwamuzi anakamilisha kipindi cha kwanza.
Dakika 45: Mwamuzi anaonyesha dakika mbili za nyongeza.
Dakika ya 43: Yanga wanatengeneza nafasi lakini shuti linatoka nje.
Dakika ya 42: Kasi ya mchezo imepungua kiasi. Mtibwa wanaonekana kuwa makini katika kuzuia kufungwa.
Dakika ya 38: Mchezo ni mgumu kwa timu zote na zinashambuliana kwa zamu. Donald Ngoma yupo chini akitibiwa baada ya kugongana na beki wa Mtibwa.
Dakika ya 33: Mtibwa wanalishambulia lango la Tanga.
Dakika ya 28: Yanga wanapata kona ya tatu lakini mpira unaokolewa na inakuwa faulo kuelekea kwa Yanga.
Dakika ya 20: Matokeo bado ni 0-0, Yanga wamefanya shambulizi kali langoni mwa Mtibwa.
Dakika ya 11, Mohammed wa Mtibwa anaachia shuti kali nje ya 18 lakini mpira unatoka nje, inakuwa goal kick
Dakika ya 11, Kiungo Dilunga anaingia lakini Dante anafanya kazi ya ziada kuokoa
Dakika ya 10, Makarani wa Mtibwa Sugar anaachia shuti lakini si kali. Mtibwa Sugar wanafika mara kadhaa, lakini mashuti yao mengi ni butu
Dakika ya 8, Stamili Mbonde anageuka vizuri kabisa mbele ya Yondani, anaachia mkwaju lakini unaokolewa
Dakika ya 6, Makapu anapoteza mpira na Mohamed anaachia mkwaju mkali langoni mwa Yanga lakini hakulenga lango
Dakika ya 5 sasa, Yanga wanaonekana kuutumia upande wa Gadiel kusukuma mashambulizi lakini Mtibwa Sugar wanacheza katikati zaidi
Dakika ya 2, Gadien anagongeana vizuri na Ajib, lakini ndani ya 18 anaanguka na mwamuzi Abdallah Kambuzi anasema twendweee
Dakika ya 1, Mtibwa Sugar wanakuwa wa kwanza kufika katika lango la Yanga lakini Rostand yuko makini, anaokoa
Dakika ya 1, Mchezo umeanza kwa kasi na Chirwa anaanza kwa kucheza madhambi dhidi ya Baba Ubaya.
Mashabiki ni wengi kwenye Uwanja wa Uhuru, hasa wale wa Yanga ndiyo ambao wamekuwa na nguvu kubwa ya kushangilia.
Timu zote zimeshaingia uwanjani kwa ajili ya mchezo huu wa Ligi Kuu Bara, mchezo huu unachezwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

0 comments :
Post a Comment