News
Loading...
Image Map HII NI 24 RADIO SIKILIZA NA UTUTUMIE SMS KWENDA 0684 666320 KUHUSU UNAVYOTUSIKIA

Friday, 1 September 2017

JE SAMATTA ATAWEZA KUCHEZA BAADA YA KUUMIA JANA NA KUSHINDWA KUENDELEA NA MAZOEZI MSIKILIZE DK WA TIMU YA TAIFA HAPA!!


Nahodha wa Taifa Stars Mbwana Samatta ambaye ni mshambuliaji wa klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji, leo August 31, 2017 hakuweza kumaliza hadi mwisho mazoezi pamoja na wachezaji wengine wa timu ya taifa wanaojiandaa kwa mchezo wa kirafiki dhidi ya Botswana.
Wakati mazoezi yanaelekea ukingoni, Samatta aliumia eneo la kisigino cha mguu wa kushoto na kulazimika kutoka nje ya uwanja kupatiwa huduma ya kwanza na madaktari wa timu.
Baada ya kumalizika kwa mazoezi tulizungumza na daktari wa timu Gilbert Kigadya ili kujua Samatta anasumbuliwa na nini na kama atakuwa miongoni mwa wachezaji watakaocheza mechi ya Jumamosi dhidi ya Botswana.
“Tatizo lake dogo tu, ameugonga mguu chini wakati anarudisha baada ya ku-serve mpira kwa hiyo wakati anarudisha mguu chini akaugonga kwa hiyo ni maumivu madogo. nina uhakika hadi kesho atakuwa vizuri,” Kigadya.
Stars itacheza dhidi ya Botswana Jumamosi September 2, 2017 mchezo wa kirafiki wa kalenda ya FIFA kwenye uwanja wa Uhuru, Dar.
* USISAHAU KULIKE PAGE YETU HAPA*
Share on Google Plus

About

0 comments :

Post a Comment