News
Loading...
Image Map HII NI 24 RADIO SIKILIZA NA UTUTUMIE SMS KWENDA 0684 666320 KUHUSU UNAVYOTUSIKIA

Friday 25 August 2017

ZLATAN IBRAHIMOVIC AREJEA MAN UNITED, ASAINI MWAKA MMOJA



Manchester United imemuongezea mkataba wa mwaka mmoja mshambuliaji mkongwe  Zlatan Ibrahimovic.
Ibrahimovic alikuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha miezi mitatu kutokana na kusumbuliwa na jeraha la goti alilolipata tangu Aprili 28.
Mchezaji huyo wa Old Trafford aliifungia timu hiyo jumla ya mabao 28 katika michezo 46 aliyocheza msimu uliyopita.
Mara baada ya kusajiliwa Ibrahimovic mwenye umri wa miaka 35 amesema “Nimerudi United kumalizia kile nilichokianza,” amesema Zlatan Ibrahimovic.
“Kamwe siwezi kuondoka katika dimba la Old Trafford na kwa sasa nitatumia muda wangu wakutosha ilikujiweka sawa”.
Mchezaji huyo sasa atakuwa akivaa jezi namba 10 ambayo ilikuwa ikivaliwa na Wayne Rooney aliyejiunga na Everton.

* USISAHAU KULIKE PAGE YETU HAPA*
Share on Google Plus

About

0 comments :

Post a Comment