Manchester United imeanza mazungumzo ya kutaka kumsajili staa Zlatan Ibrahimovic.
Awali Zlatan aliitumikia timu hiyo kwa mafanikio makubwa msimu uliopita, lakini mwishoni akakumbwa na majeraha na United kumweka kati ya wachezaji walioachana nao.
Hata hivyo, pamoja na kwamba anatarajiwa kukaa nje hadi mwezi Januari mwakani, United wameanza tena mazugumzo ya kuhakikisha wanamsajili kwenye timu hiyo.
Awali taarifa zilisema kuwa anaweza kuondoka na kwenda kujiunga na timu za Marekani lakini mwenyewe alikiri kuwa anataka kubaki kwenye Ligi Kuu ya England.
Ibrahimovic ameshafunga mabao 17 kwenye michezo 28 ya Ligi Kuu England ambayo aliitumikia United msimu uliopita.
United wamesema kuwa watakuwa tayari kumsajili upya pale tu atakapokuwa amepona vizuri.



0 comments :
Post a Comment