Kocha wa zamani wa Tanzania, Taifa Stars Mbrazili, Marcio Maximo amemtaja rais anayestaili kuchukua nafasi ya Jamali Malinzi ni Fredrick Mwakalebela.
Kauli hiyo, aliitoa ikiwa ni siku moja kabla ya uchaguzi huo wa TFF ufanyike Jumamosi hii mkoani Dodoma.
Maximo alionekana kutoa mapendekezo hayo kupitia moja ya video akimzungumzia Mwakalebela.
Katika video hiyo, Maximo alisikika akisema kuwa "Binafsi rais anayestaili kwa hivi sasa TFF ni Mwakalebela pekee kutokana na utendaji wake kazi.
"Nakumbuka Mwakalebela alikuwa katibu kipindi cha rais Tenga (Leodegar) ambaye ni rais bora kabisa aliyeweza kuliongoza vema shirikisho.
"Hivyo, kutokana na ubora huo wa Tenga ninaamini Mwakalebela atakuwa anaiga utawala bora kupitia kwa Tenga aliyeweza kuliendelesha shirikisho hilo kwa mafanikio, hivyo ninawashauri wapiga kula wamchague Mwakalebela," alisikika Maximo aliyewahi kuifundisha Yanga.



0 comments :
Post a Comment