FULL TIME
Simba imepata ushindi wa penati 5-4 baada ya matokeo ya 0-0. Waliokosa penati upande wa Yanga ni Kelvin Yondani na Juma Mahadhi, aliyekosa wa Simba ni Mohamed Hussein 'Zimbwe Jr'.
Dakika 90 za mchezo wa Yanga dhidi ya Simba zimekamilika, sasa ni muda wa timu hizo kupigiana penati.
Mwamuzi anakamilisha dakika 90 za mchezo huu. Anapuliza filimbi kumaliza kipindi cha pili.
Dakika ya 93: Muda wowote mchezo unaweza kumalizika kwa dakika za kawaida kukamilika.
Dakika ya 91: Simba wanapata kona lakini inakuwa haina faida.
Dakika 90: Mwamuzi anaongeza dakika 3 za nyongeza.
Dakika ya 89: Ajibu anaingia karibu na lango la Simba anazuiliwa.
Dakika ya 88: Mchezo umeanza kuwa wa presha, mashabiki wamepunguza kushangilia.
Dakika ya 87: Yanga wanamtoa Juma Abdul anaingia Hassan Kessy.
Dakika ya 86: Kelvin Yondani wa Yanga anapata kadi ya njano.
Dakika ya 82: Beki wa Yanga, Andrew yupo chini akipatiwa matibabu.
Dakika ya 79: Yanga wanafanya shambulizi kali lakini inakuwa off side.
Dakika ya 78: Simba wanamtoa Mzamiru anaingia Mohamed Ibrahim 'Mo', anaingia kwa kucheza vizuri lakini Yanga wanakuwa makini.
Dakika ya 76; Mchezo unaendelea kwa kasi.
Dakika ya 74: Yanga wanafanya mabadiliko, anatoka Raphael Daud anaingia Juma Mahadhi.
Dakika ya 72: Simba wanafanya mabadiliko, anatoka Mavugo, anaingia Juma Liuzio.
Dakika ya 71: Yanga wanafanya shambulizi kali.
Dakika ya 67: Gadiel anaingia na mpira na kupiga krosi lakini inapaa juu.
Dakika ya 64: Yanga wanajipanga wakipiga pasi kadhaa Simba nao wanachukua na kupiga pasi kadhaa.
Dakika ya 60: Matokeo bado 0-0, mchezo ni mkali kwa timu zote kushambuliana kwa zamu.
Dakika ya 57: Okwi anapata nafasi ya kufunga lakini anashindwa akiwa yeye na kipa.
Dakika ya 55: Mchezo umeongezeka kasi, Yanga wameanza kucheza vizuri kwa kumiliki mpira tofauti na kipindi cha kwanza.
Dakika ya 50: Haruna Niyonzima anapewa kadi ya njani, anamlalamikia mwamuzi wa kati.
Dakika ya 48: Simba wanafanya shambulizi kali kupitia kwa Mavugo lakini mpira unatoka nje.
Dakika ya 45: Mchezo umeanza kwa mwendo wa taratibu.
Kipindi cha pili kimeanza
Timu zinaingia uwanjani kwa ajili ya kipindi cha pili.
MAPUMZIKO
Dakika ya 47: Mwamuzi anakamilisha kipindi cha kwanza, timu zote zinaenda kupumzika.
Dakika ya 45: Mwamuzi wa akiba anaonyesha dakika 2 za nyongeza.
Dakika ya 43: Hakuna timu iliyofanya shambulizi kali. Mchezo bado ni wa kushambuliana kwa zamu.
Dakika ya 40: Yanga wanapata kushambulia lakini Juma Abdul anazuiwa na Nyoni.
Dakika ya 38: Juma Abdul wa Yanga anapata kadi ya njano kwa kumchezea faulo Kotei, Niyonzima anaipiga faulo lakini inakuwa haina faida.
Dakika ya 38: Kotei anamiliki mpira katika ya uwanja, anampigia Niyonzima, Simba wanashambulia lakini Yanga wanazuia.
Dakika ya 37: Simba wanapata kona, inapigwa lakini walinzi wa Yanga wanaokoa.
Dakika ya 35: Niyonzima anaingia na mpira lakini inakuwa fualo baada ya kuunawa mpira.
Dakika ya 33: Nahodha wa Simba, Mwanjali anapewa kadi ya njano kwa kuudundisha mpira kwa hasira.
Dakika ya 30: Niyonzima anaingia na mpira lakini anachezewa faulo.
Dakika ya 27: Mchezo unaendelea kwa timu zote kushambuliana kwa zamu.
Dakika ya 26: Simba wanapiga pasi nyingi lakini Yanga wakipata wanacheza kwa kasi kushambulia.
Dakika ya 24: Ajibu anawatoka walinzi wawili wa Simba lakini anapoteza mpira.
Dakika ya 21: Mchezo unaendelea kwa kasi.
Dakika ya 19: Niyonzima anamgeuza beki wa Yanga, Gadiel Michael, anatoa pasi kwa Okwi ambaye anapiga shuti linalopaa juu ya lango.
Dakika ya 17: Simba wanatengeneza nafasi lakini bado wanashindwa kufika langoni mwa Yanga.
Dakika ya 15: Mpira unachezwa zaidi katikati ya uwanja, viungo wanafanya kazi kubwa.
Dakika ya 11: Mchezo unakuwa na kasi kubwa.
Dakika ya 9: Simba wanakuwa wazito kufanya maamuzi, Yanga wanafika langoni mara kadhaa.
Dakika ya 8: Yanga wanamiliki mpira na kutengeneza njia za kufunga lakini wanashindwa kutumia nafasi.
Dakika ya 6: Simba wanafika langoni mwa Yanga.
Dakika ya 5: Yanga wanapata kona lakini wanashindwa kuitumia vizuri.
Dakika ya 4: Ibrahimu Ajibu anachezewa faulo na beki wa Simba, Mbonde nje ya eneo la 18 wakati akielekea golini. Inakuwa faulo/
Dakika ya 2: Simba wanamiliki mpira muda mwingi, wanapiga pasi nyingi eneo lao.
Shangwe ni nyingi kutoka pande zote, idadi ya mashabiki ni kubwa.
Mchezo umeanza.
Timu zinaingia uwanajani, muda wowote mchezo utaanza.
Yanga ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom msimu uliopita, wapo uwanjani kukipiga dhidi ya Simba ambao ni mabingwa wa Kombe la FA katika mchezo wa Ngao ya Jami kuukaribisha msimu wa 2017/18.
Kikosi cha Simba kinachoanza leo
1. Aishi Manula
2. Ally Shomari
3. Erasto Nyoni
4. Salim Mbonde
5. Method Mwanjale
6. James Kotei
7. Shiza Kichuya
8. Mzamiru Yassin
9. Laudit Mavugo
10. Emanuel Okwi
11. Haruna Niyonzima
WALIOPO BENCHI
1. E. Mseja
2. M. Tshabalala
3. Juuko M
4. J. Mkude
5. M.Kazimoto
6. J Luizio
7.MO Ibrahim
Kikosi cha Yanga
1.Rostand Youthe
2. Juma Abdul
3. Gadiel Michael
4. Andrew Vicent
5. Kelvin Yondani
6. Papy Tshishimbi
7. Raphael Daud
7. Thaban Kamusoko
9. Ibrahim Ajibu
10. Donald Ngoma
11. Emmanuel Martin
WALIOPO BENCHI
Ramadhani Kabwili, Hassan Kessy, Haji Abdallah, Mwinyi Haji, Juma Makapu, Yusuph Mhilu, Juma Mahadhi
* USISAHAU KULIKE PAGE YETU HAPA*
0 comments :
Post a Comment