News
Loading...
Image Map HII NI 24 RADIO SIKILIZA NA UTUTUMIE SMS KWENDA 0684 666320 KUHUSU UNAVYOTUSIKIA

Wednesday 23 August 2017

WATOTO WA KITANZANIA WAENDA MAN CITY KUFANYA MAJARIBIO



DAR ES SALAAM, TANZANIA,24 AUGUST 2017, Waziri wa michezo nchini Tanzania Mh. Dk Harrison Mwakyembe amewatakia safari njema watoto waliochaguliwa na kampuni ya Tecno mobile kwenda kufanya majaribio  ya kucheza mpira wa miguu  katika academy ya klabu ya Manchester City nchini Uingereza. 
Akiongea katika hafla hiyo fupi kutambulisha mbele ya waziri mpango huo, Afisa Mahusiano wa Kampuni ya Tecno Mobile Bwana, Eric Mkomoya alisema kua kampuni ya Tecno Mobile ndio wadhamini pekee wa safari hiyo kupitia simu yao mpya Tecno Camon Cx toleo maalumu la machester city ambapo watoto hao wawili wataenda kupewa mafunzo yenye kiwango cha kimataifa lakin pia  endapo watafanya vizuri wanaweza kuchaguliwa kuendelea kucheza katika klabu hiyo.
picha(wadhamini wakuu wa safari hiyo Afisa Mahusiano wa Tecno Mobile Eric Mkomoya wa kwanza kushoto, meneja Masoko Franck Luo, wa kwanza kulia) 
Alisemaa .  ” Tumefurahi kukutana na serikali hasa Waziri wa michezo na kuamua kuwapa Baraka zake vijana wetu wanaokwenda huko wataondoka usiku wa tarhe 23 na kurudi tarehe 30 mwezi  wa nane”.
Akikaribishwa na mkurugenzi wa michezo, waziri wa michezo Dk. Harrison Mwakyembe amesema kua serikali ina furaha kuona wadau wanajitokeza kukuza vipaji nchini Tanzania, hasa kwa wadodo wanaochipukia. 
Dk Harrison Mwekyembe pia amesema “niwaombe wadau katika sekta ya michezo tushirikiane katika kukuza michezo, nawashukuru kampuni ya Tecno Mobile kwa kuonesha juhudi za wazi katika kufanikisha hili, serikali pia inafanya jitihada kwa nafasi kuhakikisha viwango vya soka na michezo kwa ujumla vinakua.”alimaliza. 
picha(Mh. Waziri  wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe akiwa katika picha ya pamoja na watoto  wawili  Daudi Damasi na Malimi Majaliwa wanaokwenda kufanya Majaribio,)
Mzazi wa mtoto mmojawapo  Malimi, Majliwa Mbasa amesema ana furaha kuona kijana wake amepata nafasi hiyo ana amini atafanya vizur ili afungue milango kwa vijana wengine wadogo wa kitanzania walioko nchini waweze kwenda kucheza soka la kulipwa nchini uingereza. 
Watoto wawilli Daudi Damasi pamoja na Malimi Majaliwa wanaocheza nafasi ya kipa na ushambuliaji wamepata  nafasi hizo  kutokana na ushirikiano wa Tecno Mobile na asasi ya michezo ya Magnet, watoto hao ambao wote wana miaka kumi na mbili wataondoka  kuelekea manchster city mnamo tarehe 23 mwezi wa nane na kurudi nchini tarehe 30. 
picha(Wazazi na walezi wa vijana wanaokwenda Manchester city wakiwa katika picha ya pamoja na wadhamini  wakuu kutokea  Tecno Mobile.)
matukio katika picha
(Mh. Waziri  wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe akipokea zawadi za michezo kutoka kwa Meneja Masoko wa Tecno Mobile Frank Luo.)
(Malimi Majaliwa wa kwanza kushoto na Daudi DAmasi wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kupewa Baraka  za safari na Mh. Waziri  wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe 
* USISAHAU KULIKE PAGE YETU HAPA*
Share on Google Plus

About

0 comments :

Post a Comment