News
Loading...
Image Map HII NI 24 RADIO SIKILIZA NA UTUTUMIE SMS KWENDA 0684 666320 KUHUSU UNAVYOTUSIKIA

Wednesday, 23 August 2017

UCHAMBUZI MAKINI MECHI YA SIMBA VS YANGA MECHI HII ITAMALIZWA NA HAWA HAPA....

MIAMBA ya Soka Tanzania Simba na Yanga itakutana leo katika mchezo wa ngao ya hisani ambao unasubiriwa kwa hamu kubwa na wadau wa soka ndani na nje ya nchi. Mchezo huo ni ufunguzi wa ligi msimu wa 2017/18.
Hamu kubwa ya mashabiki wa timu hizo ni kuona nini kitafanywa na nyota wawili Haruna Niyonzima wa Simba na Ibrahim Ajib wa Yanga. Hii ni kutokana na wakali hao kubadilishana timu msimu huu kwa usajili wa kishindo.
Nyota hawa wawili wanasifika kwa uwezo mkubwa wa kuuchezea mpitra na kuleta burudani kwa mashabiki. Niyonzima baada ya kumaliza mkataba na wanajangwani hao aliamua kujiunga na Simba jambo sawa na lililotokea kwa mshambuliaji Ajib.
Wakati macho na masikio ya mashabiki yakiwa kwao, nyota hao wanapaswa kujiandaa kisaikolojia kwani ni wazi kila mmoja atakutana na zomea zomea toka kwa wanazi wa timu pinzani.
Mashabiki wa Simba hawakufurahishwa na jinsi jinsi Ajib alivyoondoka katika timu yao hasa baada ya uongozi wao kukiri hadharani kuwa straika huyo ameshindwa kukubaliana na dau alilopewa ili asaini mkatabna mpya.
‘Filamu’ hiyo inafanana kila kitu na ile ya Niyonzima kuondoka Yanga kwani mara kadhaa uongozi wa mabingwa hao ulifanya jitihada za kumpa mkataba mpya lakini raia huyo wa Rwanda alishikilia msimamo wake hadi mwisho alipokubaliana na dau la Simba.
Licha ya chachu itakayoletwa na wawili hao, kuna mambo mengine kadhaa yanaweza kuongeza utamu wa mechi hii.
                                   ‘DOGO’  KABWILI KUCHEZA DERBY?
Ni  wazi kocha George Lwandamina atamtumia kipa Mcameroon Youthe Rostand katika pambano hilo, lakini mlinda mlango kinda Ramadhan Kabwili anabakia kuwa kipa pekee msaidizi na anaweza kupata nafasi ya kucheza endapo kitatokea chochote cha kumfanya Rostand ashindwe kuendelea na mchezo.
Kabwili 17, ameonyesha uwezo mkubwa katika kikosi cha timu ya taifa ya vijana ‘Serengeti Boys’ huku akisajiliwa na Yanga akiwa golikipa namba tatu lakini kuumia kwa Beno Kakolanya kumempa nafasi ya kukaa benchi.
                   LWANDAMINA AKIJILIPUA ANAWEZA KUWAAMINI VIJANA

Katika michezo ya kirafiki ambayo Yanga imecheza kujiandaa na ligi wachezaji vijana Maka Edward, Said Mussa, Burhan Akilimali na Raphael Daud wameonyesha uwezo mkubwa lakini kulingana na presha ya mechi huenda kocha Lwandamina akahofia kuwatumia.
Hata hivyo kama Lwandamina ataamua kujilipua bado makinda hao wanaweza kuwashangaza watu. Maka ameonyesha uwezo mkubwa katika kiungo mkabaji huku akionyesha uwezo mkubwa wa kupiga pasi ndefu wakati Akilimani na Said Musa wakifanya vizuri katika winga mbali na Raphael ambaye uwezo wake unajulikana tangu akiwa Mbeya City na timu ya Taifa.
                        BOCCO KUENDELEZA UBABE KWA YANGA?
Mshambuliaji wa zamani wa Azam FC John Bocco amekuwa na rekodi nzuri ya kuzifunga timu za Simba na Yanga kila anapokutana nazo. Safari hii Bocco atakutana na Yanga akiwa na jezi ya Simba, swali ni je ataweza kuendeleza rekodi yake kesho ni kusubiri na kuona.
                            MTIHANI WA KWANZA KWA OMOG
Baada ya usajili wa kishindo, matumaini waliyonayo mashabiki wa Simba kwa kikosi chao ni makubwa mno kiasi kwamba matokeo yoyote mabaya kwa wekundu hao yatawafanya wahamishie lawama kwa kocha Joseph Omog.
Simba imesajili mastaa kadhaa kama Emmanuel Okwi, Niyonzima, Bocco, Aishi Manula, Erasto Nyoni, Ally Shomari, Yusuph Mlipili na Jamal Mwambeleko hivyo endapo Wekundu hao watapoteza mchezo huo Omog anaweza kujikuta katika mazingira magumu kubebeshwa zigo la lawama.
                                          MWAMUZI KIJANA MIAKA 28
Bodi ya ligi ya Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) imemteua Elly Sasii 28, kuchezesha mchezo huo mkubwa utakaoanza saa 11 jioni kwenye uwanja wa Taifa.
Sasii atasaidiwa na Ferdinand Chacha na Helen Mduma wakati Israel Nkongo akiwa mwamuzi wa akiba.
USISAHAU KULIKE PAGE YETU HAPA*
Share on Google Plus

About

0 comments :

Post a Comment