News
Loading...
Image Map HII NI 24 RADIO SIKILIZA NA UTUTUMIE SMS KWENDA 0684 666320 KUHUSU UNAVYOTUSIKIA

Sunday, 20 August 2017

ULIMBOKA ASHINDWA KUVUMILIA ,AINGIWA HOFU UKAME WA MABAO SIMBA ASIKITIKA ASEMA......

Tokeo la picha la Ulimboka Mwakingwe
Dar es Salaam. Wakati homa ya mchezo wa Ngao ya Jamii kati ya Yanga na Simba ikipanda, mchezaji wa zamani wa Simba, Ulimboka Mwakingwe amemtaka Kocha Joseph Omog kuwa makini na safu ya ushambuliaji.
Timu hizo zitakutana Agosti 23, kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii utakaofanyika kwenye Uwanja wa Taifa utaashirikia ufunguzi wa Ligi Kuu msimu wa 2017/18.
Mwakingwe alisema ameshtushwa na hatua ya washambuliaji wa Simba kufunga mabao matatu katika mechi za kirafiki na kumtaka kocha Joseph Omog kulifanyia kazi eneo hilo.
“Sielewi ni mipango ya kocha au la, lakini msimu uliopita Simba walikosa ubingwa kwa idadi ndogo ya magoli, mwalimu aliangalie hilo,” alieleza Mwakingwe.
Mashabiki wa Simba wameingiwa na hofu baada ya safu ya ushambuliaji kufunga mabao matano katika mechi nne za kirafiki ilizocheza dhidi ya Orlando Pirates, Bidvest Wits, Polisi Dar, Mtibwa Sugar, Rayon Sports na Mlandege.
Hata hivyo, Mwakingwe alisema hana wasiwasi na safu ya ulinzi aliyodai itahimili vishindo vya washambuliaji wa timu pinzani.
* USISAHAU KULIKE PAGE YETU HAPA*
Share on Google Plus

About

0 comments :

Post a Comment