Kuelekea mchezo wa Ngao ya Jamii kati ya Yanga dhidi ya Simba, Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) limetoa ufafanuzi juu ya wachezaji kadhaa waliosimamishwa kucheza.
Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas amesema kuwa Yanga hitaweza kumtumia Obrey Chirwa kwa kuwa ana kesi ambayo imesababisha asimamishwe yeye na wenzake.
Alfred amesema licha ya kuwa Yanga imedai kuwa Chirwa ataukosa mchezo huo kwa kuwa ni majeruhi, lakini hata kama angekuwa fiti bado hasingepata nafasi ya kucheza kwa kuwa katika mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu ya Vodacom akiwa na wachezaji wenzake wa Yanga, walifunguliwa mashitaka katika Kamati ya Nidhamu.
Amesema walifunguliwa kesi hiyo kutokana na kumsukuma mwamuzi wa mchezo huo wa mwisho, hivyo Chirwa amesimamishwa akisubiri maamuzi ya kamati hiyo, wengine waliokumbwa na adhabu hiyo ni Deus Kaseke ambaye kwa sasa yupo Singida United pamoja na Simon Msuva ambaye kwa sasa yupo nje ya nchi akicheza soka la kulipwa Morocco.
Alfred amesema ikiwa kamati hiyo haitakutana hadi kufikia Jumamosi basi wachezaji hao Chirwa na Kaseke hawataweza kucheza mechi za ufunguzi wa ligi hiyo, lakini kamati ikikutana watasubiri maamuzi yatakayotolewa kwa wote watatu msuva yeye Rungu la kusimamishwa kucheza limemuepuka kwa sababu anacheza nje.
* USISAHAU KULIKE PAGE YETU HAPA*
0 comments :
Post a Comment