
Kiungo wa zamani wa klabu ya Liverpool, Steven Gerrad amezungumzia juu ya uvumi unaomuhusisha nyota wa klabu hiyo (Liverpool) Philippe Coutinho kutimkia katika klabu ya FC Barcelona ya nchini Hispania kwa kusema kuwa:-
“Ngumu sana kwa wachezaji wanaotoka Amerika Kusini kukataa kujiunga na klabu kama vile Barcelona na Madrid kwasababu ndiyo ndoto zao kuwepo ndani ya klabu hizo…nasema hivyo kwani nina uzoefu nao….nimekuwanao ndani ya Liverpool ….kwa mfano Javier Mascherano, Luis Suarez …walikuwepo Liverpool lakini, wakatimkia Barcelona”. Gerrad alisema.
‘Ingawa kocha Jurgen Klopp na viongozi wengine wanasisitiza kuwa Coutinho hatouzwa msmimu huu…lakini bado koundoka au kutoondoka ni maamuzi ya mchezaji mwenyewe……..najua kinachoondelea ndani ya Liverpool kwa hivi sasa ni kutumia nguvu kubwa kumbakisha Phillippe……kitu ambacho ni kigumu sasa“. Gerrad alisisitiza.
Taarifa kutoka Uingereza zinasema maafisa wa klabu ya FC Barcelona waliwasili uingereza na kuweka wazi kuwa wapo tayari kutoa kitita cha paundi million 122 ili kuinasa nsaini ya Philippe Coutinho kabla ya dirisha la Usajili kufungwa mwezi huu.

Barcelona inapigania saini ya nyota huyo wa Liverpool ili kuziba nafasi aliyoiacha Neymaraliyetimkia klabu ya PSG ya Ufaransa kwa dau la paundi millioni 198.



0 comments :
Post a Comment