Wakati wapenzi wa SIMBA wakiwa na furaha kuhusiana na Tamasha la Simba Day lilivyokwenda na matokeo yake ikiwa pamoja na kuwaona wachezaji wao wapya waliosajiliwa na ikiwemo na matokeo ya mtanange uliopigwa siku ya simba Day lakini kuna kitu kimoja kilichotokea ambacho kiliwaacha hoi wapenzi wa soka Tanzania ikiwa ni kinyume kabisa za utaratibu wa vilabu hivi viwili ambapo mchezaji ambae aliondoka Simba msimu huu huu akaenda kwa mahasimu wao YANGA Ibrahim Ajib kwenda kwenye SIMBA DAY huku sakata lake likiwa hata halijaisha vizuri tumeshuhudia vijembe ambavyo Ajib anavitoa Twitter pia tumekua tukishuhudia pia Msemaji wa Simba Haji Manara vijembe alivyokua akivitoa kwake acha matusi na kashfa ambazo Ajib anavipata kila siku kwenye mitandao ya kijamii hasa Facebook kwenye Group za mashabiki wa simba lakini Ajibu akaenda, je ni kipi ambacho kilimsukuma Ibrahim Ajibu aende bila kuogopa ajira yake mpya ambayo hata hajaanza kuitumikia kwenye mechi za ligi? katika kuchimbua swala hili
MWANASPORTS LEO
lilipata jibu kwa mtu ambae hakutaka kutajwa jina lake kua ule ulikua mpango wa kikosi cha Yanga
kuwasoma wapinzani wao na mtu anaekifahamu vizuri kikosi hicho ni Ibrahim Ajibu kwa hio lile lilikua jicho la YANGA kuwasoma SIMBA na kufahamu udhaifu na uimara wao na YANGA wamefanikiwa kwa hilo wakati mashabiki wa SIMBA wakichekelea ooooh! Ajibu ameanza kuimiss SIMBA kumbe Ajib amefika na yake na amepata alichokitaka na kukipeleka kwa kocha wake Lwandamina hivi mpenzi msomaji wa blog hii ya
Mwanasports leo nadhani unazijua timu hizi mbili zilivyo tena wakiwa wanakaribia mechi baina yao ingekua Ajib ameenda tu mwenyewe angekua na kibarua leo hii YANGA? au viongozi wa timu ya YANGA wangekaa tu kimya kama hivi Haji Manara anapiga madongo wao wamekaa kimya bila kuongea chochote huku kukiwa na ushahidi wa picha kila sehemu? mpira ni mipngo na kwenye hili YANGA wamewini sasa tuone je ujanja waoutawasaidia tarehe 23 watakapokutana?
0 comments :
Post a Comment