Klabu ya Ruvu Shooting ya mkoani Pwani imesema kuwa imetumia mchezo wa Ngao ya Jamii kuwasoma wapinzani wao Simba kwa ajili ya mchezo wao wa kesho Jumamosi katika ufunguzi wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2017/18.
Akizungumza jijini Dar, Ofisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire alisema kocha mkuu wa timu hiyo Abdulhumud Haji ametumia mchezo huo kuwasoma wapinzani wao ipasavyo ambapo atazifanyia kazi mbinu zao ili kushinda mchezo huo.
“Kocha wetu mkuu Abdulhumud Haji aliifuatilia Simba kwa ukaribu, tunahitaji Watanzania waone jinsi tunavyofanya ili wawe na imani na timu yetu kutokana na kushinda mchezo huo kwani tutakuwa na heshima kutokana na timu tutakayokutana nayo ndiyo ipo juu kwa sasa.
“Kikosi chetu kipo vizuri, wachezaji wamecheza mechi kadhaa za kirafiki ambapo kila mmoja ameweza kuona jinsi vijana walivyopambana hivyo tuna imani ya kufanya vizuri kwenye ligi,” alisema Masau
0 comments :
Post a Comment