Licha ya Klabu ya Simba kusema kuwa wanachama wa klabu hiyo wamepitisha kwa nguvu moja mabadiliko ya uongozi klabuni hapo, mzee Hamis Kilomoni ameibuka na kusema neno.
Simba ilipitisha maamuzi hayo jana kwenye mkutano wa wanachama wake uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, na sasa inaelekea kwenye hatua nyingine ya kufuata mchakato wa kubadilisha uendeshaji wa klabu hiyo kuwa katika mfumo wa hisa.
Mzee Kilomoni ambaye ni mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini wa Klabu ya Simba, amesema anatarajiwa kutoa tamko leo Jumatatu juu ya msimamo wake kwa kuwa bado hajapata taarifa rasmi juu ya maamuzi hayo ya mkutano huo.
Mzee Kilomoni ambaye alisimamishwa uanachama na kuondolewa kwenye nafasi hiyo ya baraza la wadhamini, siku chache zilizopita alishakiri kuwa hatambui maamuzi hayo kwa kuwa yeye ni mmoja wa waasisi halisi wa Simba na hakupewa cheo hicho kama zawadi.
* USISAHAU KULIKE PAGE YETU HAPA*
0 comments :
Post a Comment