Baada ya timu yake kufungwa mabao 2-0 na kulikosa taji la Spanish Super Cup kutoka kwa Real Madrid, hatimaye beki mkongwe wa Barcelona, Gerard Pique amekiri kwa mara ya kwanza ameona timu yake ikizidiwa na wapinzani wao hao.
Pique amesema kwa mara ya kwanza ameshuhudia Barcelona ikizidiwa mbali na Madrid katika miaka yake yote aliyocheza klabuni hapo licha ya kuwa imeshawahi kupoteza michezo kadhaa kutoka kwa Madrid.
"Msimu bado ni mrefu na kuna nafasi ya kuboresha kikosi, hii ndiyo mara ya kwanza nimeona tukiwa wadogo na wao wana nguvu, lakini tutapambana,” alisema Pique
* USISAHAU KULIKE PAGE YETU HAPA*



0 comments :
Post a Comment