Ofisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire ambaye timu yake ilifungwa mabao 7-0 na Simba, Jumamosi iliyopita, ameibuka na kuzungumzia bao lililofungwa na mshambuliaji wa Yanga, Donald Ngoma.
Yanga ilipata sare ya bao 1-1 dhidi ya Lipuli FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, lakini bao alilofunga Donald Ngoma lilizua utata kwa kuonekana kama halijavuka mstari wa golini.
Bao hilo lililalamikiwa na wachezaji na benchi la ufundi la Lipuli lakini mwamuzi aliamuri liwe bao.
Akizungumzia tukio hilo, Masau Bwire alisema yeye aliona bao hilo na aliona mpira umevuka mstari wa golini, hivyo ni bao halali.
* USISAHAU KULIKE PAGE YETU HAPA*
0 comments :
Post a Comment