Wimbo mbaya haubembelezewi Mwana.. Wahenga tulishatoa tamko siku nyingi..!! Wimbo huu wa Turudishie mpira wetu ndio wimbo uliokubalika na ukaimbwa na ukaimbika Vyema kabla na Kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Nafasi ya Urais na Ujumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira nchini yaani TFF. Baada ya Uchaguzi kwisha na Wimbo huu umezimwa au kuzimika ghafla. Lakini kwa wenye Akili wimbo huu bado unaimbwa na unaimbika Vyema kabisa vichwani Mwao. Hakuna ubishi kuwa wimbo huu uligeuka kuwa Wimbo wa Wananchi wa Tanzania kwa jinsi kelele zilivyokuwa zikisikika haswa Mitandaoni na kwenye Vyombo vingi vya Habari. Huu ndio wimbo uliokuwa bora zaidi kuelekea Uchaguzi ule. Hata Rais Karia anajua hilo...!!! Ubaya wa Wimbo Ule. Wimbo ule ulijaa maneno mengi yasiyo na tafsiri ya moja kwa moja hivyo kuhitaji watu wenye vichwa vipana sana kukubaliana na Tafsiri iliyokusudiwa. Wimbo ulijaa maneno mengi yasiyofafanulika kirahisi kiasi kila mtu akautafsiri ajuavyo lakini wimbo ule ulibakia kuwa Wimbo bora na Ulioogofya kuelekea Uchaguzi Mkuu wa TFF. Wengine waliutilia Mashaka kuwa wimbo ule ungewaathiri katika utekelezaji wake kwa kuwa baada ya muda fulani wenye kuudai mpira wao wangepoka nafasi zao na kuzimiliki. Hii iliogofya na kusababisha Falsafa ya 'Tujilinde Kwanza' itumike. Na ilitumika Vyema. Uzuri Wa Wimbo Ule : Wimbo ule unaishi...!!! Wimbo ule hauchuji na wala hauoneshi ipo siku utachosha watu kuuimba...!! Wimbo ule umejaa Falsafa kamili ya Uhitaji wa watu...!! Haukwepeki Kuuimba.. Utake.. Usitake... Utauimba hata Kimoyo Moyo...!!! Ngoja nifungue Mabano...!! Rais Karia amekuwepo kwenye Maisha ya Mpira wa Tanzania kwa miaka mingi mno kuliko wengi walivyodhani. Hakuwa mtu wa kujikweza wala mtu wa Vyombo vya Habari wala Mtu aliyetafuta sifa binafsi... Hapana..!!! Na ndio maana hata waliokuwa wakimpinga nje ya Ulingo walimpinga kwa hoja dhaifu kuwa yeye ni Miongoni mwa walalamikiwa kwa ''Upotevu wa Mpira wao''... Hoja Dhaifu..!!! Wajuzi na Wanaomjua Rais Karia wanasema 'Alitengwa na Mfumo'.. Lakini alikuwa ni mtu bora zaidi kiutendaji na aliamini katika mpangilio na sio 'twende tufanye'. Hii ilimfanya akae mbali na Mfumo kisha aandae kile anachokiamini kuwa ni bora zaidi kuelekea Mafanikio makubwa aliyoyatamani. Na ndio maana hakuogopa kuchukua fomu mbele ya 'Rais' wake aliyekuwa nae. Wenye kufikiri... Watajiongeza hapa...!!! Hata kilele cha Uchaguzi kilipofika tayari Wajumbe 95 kati ya Wajumbe 131 waliostahili kupiga kura walishakuwa na Maamuzi. ( Bado namtafuta Kocha Muhibu Kanu ili anipe Siri ya kupatikana kwa kura hizi.) Nilipomuona Ally Mayai Tembele na Shafih Dauda wakihojiwa.. Kwa bashasha waliyokuwa nayo... Nilihisi kabisa bado tuko salama..!!! Hawakuonesha mashaka wala hofu yoyote juu ya Mchakato... Waliridhia...!!! Ally aliibeba kauli mbiu iliyogusa hisia za Mashabiki wa Soka na ni Kauli mbiu hiyo ambayo Rais Karia anawajibika kuitekeleza kwa kuwa ndiyo hisia kamili za Mashabiki. Si dhambi...!! Tumeshuhudia hata kwenye Siasa za Nchi yetu 'Mabadiliko' yalipohitajika hayakuchagua nani kaanzisha neno hilo bali Tafsiri halisi ya kinachoitwa 'Mabadiliko' ndicho kinachoendelea kufanyiwa kazi... Si dhambi kwa Rais Karia kuijua Vyema Falsafa ya Kurudisha Mpira na Kuifanyia kazi kikamilifu hata kwa kukaa chini na Muasisi wa Kauli mbiu hiyo na kumtaka washirikiane kuitafsiri kivitendo zaidi.. Si Dhambi...!! Rais Karia yupo kwa ajili ya Watanzania wote na hadi hapo alipo ajue tu kuwa anatekeleza dhana iliyojificha kuwa ipo sehemu tunakosea au tulikosea... Atusaidie kuifichua...!! Rais Karia kwa kuwa amedhihirisha si mtu wa Makundi na wala hana 'Watu Wake'... Tunamuomba Aturudishie Mpira Wetu...!!! Rais Karia ajue hana dosari na wala asiitafute dosari abaki kuwa Baba wa Mpira na Wapenda mpira wote. Turudishie mpira wetu Mashuleni na Vyuoni uchezwe kwa Ufundi na Weledi kwa kuwa Makocha wenye Vigezo ni Wengi. Turudishie mpira wetu kwa kulazimisha uwepo wa Wakurugenzi wa Ufundi kwenye kila timu ya Ligi Kuu na Hata Daraja la Kwanza. Turudishie Mpira wetu kwa kuweka Kitengo maalum cha wataalam wa Masoko ili kushawishi Makampuni makubwa ya Ndani na Nje ya Nchi kuwekeza kwenye Soka nchini katika ngazi zote. Turudishie mpira wetu kwa kuwa na ligi zinazochezwa nchi nzima kuanzia ngazi ya Kata. Turudishie mpira wetu kwa kuwa na Soka la Mkoa kwa Mkoa ili kurudisha uwezo wa Mikoa kuwa na timu ngumu na zenye uwezo wa kushindana na timu za Kariakoo. Nina mengi ya kutaka uturudishie kwenye Soka ila najua nawe una mengi uliyopanga yarudi kwenye Soka!!!.
Slogan Covered...!!!
Nawasilisha.
Imeandikwa na Chiki Mchoma +255 712 885 999.
* USISAHAU KULIKE PAGE YETU HAPA*
0 comments :
Post a Comment