News
Loading...
Image Map HII NI 24 RADIO SIKILIZA NA UTUTUMIE SMS KWENDA 0684 666320 KUHUSU UNAVYOTUSIKIA

Wednesday, 9 August 2017

MAJIBU YA HARUNA NIYONZIMA: NILIPOMUULIZA JE UNATAMANI KUWAFUNGA YANGA NA UKIFUNGA UTASHANGILIA ? SIKILIZA JIBU LAKE NA HUTAAMINI...

Mchezaji Mpya wa Simba Haruna Niyonzima ambaye awali alikuwa mchezaji wa Mabingwa wa Ligi Kuu VPL 2016/2017 Yanga amesema siku ya Mechi ya Ngao ya Hisani dhidi ya Yanga haitakuwa Mechi rahisi kwake ila atamuomba Mungu iwe Rahisi.

Kuhusu Kushangilia Kama Atafunga goli Siku Hiyo  amesema Kwanza Anatamani kufunga goli siku hiyo na Kushangilia atashangilia lakini kwa Heshima Kubwa.

 " Nitashangilia lakini kwa heshima nacheza na Mtu ambaye namjua nacheza na Ndugu yangu, Ofcourse Ningetamani Kufunga Goli ili niwaage kwa Heshima " alisema Mido huyo wa Kinyarwanda.

Niyonzima amecheza Yanga kwa misimu 6 mfulululizo na Msimu huu amejiunga na Simba mara baada ya kushindwa kumalizana na Klabu yake ya Yanga
Share on Google Plus

About

0 comments :

Post a Comment