News
Loading...
Image Map HII NI 24 RADIO SIKILIZA NA UTUTUMIE SMS KWENDA 0684 666320 KUHUSU UNAVYOTUSIKIA

Tuesday, 15 August 2017

KOCHA MEJA MINGANGE ASEMA SIMBA WATAKUFA AGOSTI 23 KWA YANGA KWA SABABU HII HAPA.......


NA ZAINAB IDDY

KOCHA wa zamani wa Ndanda FC, Meja Mstaafu wa Jeshi, Abdul Mingange, amesema anaipa nafasi kubwa Yanga kuibuka na ushindi katika mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Simba, itakayochezwa Agosti 23, mwaka huu, kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Akizungumza na BINGWA jana, Meja Mingange alisema Yanga wana nafasi ya kushinda katika mechi hiyo kutokana na ubutu wa washambuliaji wa Simba.
Meja Mingange alisema Yanga wana washambuliaji wanaojituma na wanawapa nafasi kubwa ya kushinda katika mechi hiyo.
“Kama si sare basi Simba inaweza kufungwa, kwani haina watu wenye shauku ya kufunga kama ilivyokuwa kwa Yanga ambayo kwa sasa inaonekana ina tatizo kwenye beki ya kati.
“Simba ina mastraika wengi, lakini wote hawana shauku ya kufunga, hivyo wingi wao hauwezi kuisaidia timu kupata mabao, labda kama watabadilika,” alisema Meja Mingange.

* USISAHAU KULIKE PAGE YETU HAPA*
Share on Google Plus

About

2 comments :

  1. Sasa umeishasema kuwa wana tatizo la beki,sasa maana yake tatizo hilo si ndiyo magoli ya Simba? Jeshi na Soka tofauti kabisa.

    ReplyDelete
  2. Sasa umeishasema kuwa wana tatizo la beki,sasa maana yake tatizo hilo si ndiyo magoli ya Simba? Jeshi na Soka tofauti kabisa.

    ReplyDelete