Kikosi cha Yanga kinaendelea na mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya wa 2017/18 kisiwani Pemba ambapo wachezaji wawili kati ya waliopo huko wameonyesha kutokwua vizuri kiafya.
Yanga inajianda na msimu ujao lakini zaidi ni mcheoz ulio mbele yao dhidi ya Simba ambao unatarajiwa kuchezwa Jumatano ijayo katika Ngao ya Jamii, Simba wao wapo kisiwani Unguja wakijiandaa kw amchezo huo pia.
Katika mazoezi ya asubuhi ya leo, Yanga ambayo imefikia katikati ya Mji wa Chake Chake, ilifanya mazoezi ya nguvu chini ya Kocha George Lwandamina lakini mshambuliaji Amiss Tambwe na winga Geofrey Mwashiuya walifanya mazoezi mepesi kutokana na kile kilichoonekana kuwa hawapo fiti kiafya.
Akizungumza juu ya kambi hiyo, meneja wa Yanga, Hafidhi alisema kweli kuna wachezaji afya zao hazipo sawa lakini kwa jumla kikosi kipo vizuri.
* USISAHAU KULIKE PAGE YETU HAPA*
0 comments :
Post a Comment