News
Loading...
Image Map HII NI 24 RADIO SIKILIZA NA UTUTUMIE SMS KWENDA 0684 666320 KUHUSU UNAVYOTUSIKIA

Thursday, 10 August 2017

HUYU NDIE "MO" HEBU MSIKILIZE ALICHO JIBU NILIPOMUULIZA JE UKIKABIDHIWA TIMU NINI HASA UNATAKA UIFANYIE SIMBA AKANINIJIBU HIVI.....


Shabiki na mwanachama wa Klabu ya Simba, Mohamed Dewji maarufu kwa jina la Mo amefunguka kuwa nia yake ni kuifanyia makubwa klabu hiyo, siyo tu Tanzania bali Afrika kwa jumla.
Mo alisema hayo alipokuwa akihojiwa wakati wa Tamasha la Simba Day lililofanyika jana kwenye Uwanja wa Taifa ambapo Simba ilicheza mechi dhidi ya Rayon Sports ya Rwanda.
Akizungumza kabla ya mchezo huo kuanza, Mo alisema anafarijika kuona Simba ina mipango mizuri, akiwa mmoja wa wanachama wa klabu hiyo nia yake ni kuona Simba inafanya vizuri kimataifa na siyo kuishia ndani ya Tanzania pekee.
Akizungumza zaidi Mo alisema: “Ni kweli nimekuwa nikijitolea ndani ya Simba, sisi Wanasimba tunapenda kuona timu yetu ikifanya vizuri kuanzia ligi za ndani hadi nje, ndiyo maana unaona hata usajili umekuwa ni wa kusajili wachezaji wazoefu.”  
Share on Google Plus

About

0 comments :

Post a Comment